DKT NDUMBARO ATAJA MANUFAA YA FEDHA ZA MKOPO KWA WANANCHI WA MKOA WA RUVUMA

 


Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro ambaye pia ni Mbunge wa Songea Mjini  akizungumza na mamia ya  Wakazi wa Songea Mjini waliojumuika kwa pamoja katika Bustani ya Wanyamapori ya Ruhila ili kusherekea sikukuu ya Mwaka Mpya ikiwa ni  jitihada za kuhamasisha utalii wa ndani 
Waziri wa Maliasili na Utalii ambaye pia ni Mbunge wa Songea Mjini  akiwa na Meya wa Manispaa ta Songea Mjini, Mhe.Michael Mbano  wakiwa wameongozana na Wakazi wa Songea Mjini mara baada ya kuwasili katika Bustani ya Wanyamapori ya Ruhila iliyopo katikati ta  Manispaa ya Songea ikiwa ni muendelezo wa kuukaribisha mwaka mpya kwa kuhamasisha wakazi wa Songea kujenga utamaduni wa kutembelea maeneo ya vivutio vya utalii.
Waziri wa Maliasili na Utalii ambaye pia ni Mbunge wa Songea Mjini, Dkt.Damas Ndumbaro akiwa na  Muendesha baiskeli wakijiandaa kuanza mashindano ya baiskeli yaliyofanyika ndani ya Bustani ya Wanyamapori ya Ruhila

…………………………………………………………..

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro amesema  Wananchi wa Mkoa wa Ruvuma  wana kila sababu ya kumshukuru na kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya ikiwemo kutoa fedha kwenye Wizara ya Maliasili na Utalii za kukarabati miundombinu ya maeneo ya vivutio vya utalii vilivyopo katika Mkoa huo.

Wito huo ameutoa wakati alipoongoza mamia ya wakazi wa Jimbo la Songea mjini kwenda kusheherekea mwaka mpya wa 2022 kwa kufanya utalii wa ndani kwa nyakati tofauti katika Msitu wa Hifadhi ya  Mlima Matogoro pamoja na Bustani ya Wanyamapori ya Ruhila  iliyopo katikati ya   Manispaa ya Songea  Mjini
Akitaja fedha manufaa ya fedha  hizo, Dkt.Ndumbaro amesema Songea ni mji uliobarikiwa kuwa na vivutio vingi vya utalii  hivyo fedha hizo za mkopo zitatumika kwa ajili ya kuimarisha miundombinu ya maeneo ya vivutio ili kuimarisha utalii
Amesisitiza kuwa Hifadhi ya Msitu wa Mlima  Matogoro ni kivutio kikubwa cha utalii katika mkoa huo isipokuwa changamoto ya barabara ndiyo imekuwa kikwazo cha watalii walio wengi kushindwa kufika
Dkt.Ndumbaro amesema kupitia fedha hizo za mkopo itajengwaa barabara ya uhakika itakayofika hadi juu ya misitu ya milima Matogoro ili kuwarahisishia wanaoenda kufanya utalii huku akisisitiza kuwa tayari Mkandarasi amepatikana na anatajiwa kukabidhiwa  eneo la ujenzi tarehe 15 Januari mwaka huu 
” Mhe.Rais ametuona na kutuamini  wana Songea kwa kutupatia fedha kwa ajili ya kutengeneza barabara ili kuhakikisha watalii watakaoamua kutumia magari yao kufika katika kilele cha Mlima huo wanaweza kufika tofauti na ilivyosasa magari madogo huku hayawezi kufika kutokana na ubovu wa barabara” alisema Dkt.Ndumbaro 
Pia, Dkt.Ndumbaro amesema Mhe.Rais Samia  Samia aliridhia kutengwa kwa bajeti ya mwaka huu ya jumla ya kiasi cha shilingo milioni 50 kwa ajili ya kukarabati uzio wa Bustani ya Wanyamapori ya Ruhila.ambayo imezidi kupata umaarufu siku za hivi karibuni baada ya kufanyika kwa maboresho makubwa
Dkt  Ndumbaro amesema kuboreka kwa miundombinu katika maeneo ya vivutio vya utalii  kutachochea Manispaa ya Songea mjini kimapato.kwa vile Utalii ni sekta mtambuka
 Hata hivyo, Dkt.Ndumbaro amewataka Wakazi wa Songea kuchangamkia fursa za utalii zilizopo katika mkoa huo huku akiwasisitiza kujenga tabia ya kutembelea maeneo ya vivutio hivyo ili kutambua fursa zilizopo kwenye maeneo yao.
Katika hatua nyingine Waziri Ndumbaro  amewataka Wananchi hao kuwa mstari wa mbele kulinda na kuhifadhi maeneo ya vivutio vya utalii badala ya kuiachia Wizara pekee ili maeneo hayo yaweze kuchochea kipato kwa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla kupitia sekta ya utalii.
Katika kusherehekea sikukuu  ya Mwaka mpya katika Bustani ya Wanyamapori ya Ruhila, Waziri Ndumbaro aliweza kuwalipia wakazi wote wa Songea Mjin i tozo zote za vingilio katika Bustani hiyo pamoja na kuhakikisha  wanakula nyama pori iliyokuwa imeandaliwa kwa ajili ya wakazi hao.

Post a Comment

Previous Post Next Post