Mkazi wa kijiji cha Mtowisa Sumbawanga Pilli Simwela akipata dozi ya kwanza ya chanjo ya UVIKO-19 aina ya Sinopharm jana wakati wa mkutano wa hadhara wa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa kuhamasisha chanjo unaofanywa kwa ushirikiano na Shirika la Walter Reed.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joseph Mkirikiti akitoa hamasa kwa wananchi wa kijiji cha Mtowisa wilaya ya Sumbawanga kuhusu umuhimu wa chanjo dhidi ya UVIKO-19
Afisa Afya wa Kituo cha Afya Mtowisa Plasidus Malapwa akitoa elimu ya chanjo ya UVIKO-19 kwenye mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa (hayupo pichani) jana. Mkoa wa Rukwa kwa kushirikiana na Shirika la Walter Reed (HJFMRI) wanaendesha zoezi la hamasa na elimu ya UVIKO-19 ili wananchi wengu wajitokeze kwa wingi