TUME YA TAIFA YA UMWAGILIAJI YATAKIWA KUTENGENEZA MFUMO WA TAARIFA ZA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YA WATUMISHI.

 Mwenyekiti wa Bodi ya Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Prof. Henry Mahoo, ameshauri Menejimenti ya Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kutengeneza Mfumo wa kiteknolojia utakaopokea taarifa za kila siku za utekelezaji wa majukumu ya watumishi kuanzia ngazi ya Wilaya, Mkoa hadi Makao makuu kwa lengo la kuboresha utendaji kazi wa Tume.

 
Akizungumza katika kikao chake na Menejimenti jijini Dodoma Prof, Mahoo amesema, mfumo huo utamsaidia Mkurugenzi Mkuu, Wakuu wa Idara na Vitengo kufuatilia utekelezaji wa majukumu ya mtumishi mmoja mmoja na kubaini mapungufu yaliyopo ama, ubora katika utendaji wake.
 
“Mfuo huo utaonyesha majukumu waliyopangiwa watumishi,utekelezaji wake, sanjari na kubadilishana taarifa baina ya viongozi wa idara na vitengo na watumishi wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji.Mfumo huo pia utasaidia katika kuboresha eneo la ufuatiliaji na tathmini ya uwajibika wa Watumishi.”
 
Aidha Prof. Mahoo amepongeza juhudi za kutanua eneo la Ofisi kwaajili ya Wataalam wa Tume na kuongeza kuwa Ofisi hizo zitabakia kuwa Ofisi za Tume Mkoa wa Dodoma mara ujenzi wa jengo la Ofisi za Makao Makuu zitakapokamilika katika eneo la Njedengwa mjini Dodoma.
 
Katika hatua nyingine Prof. Mahoo ameitaka Idara ya Uendelezaji Miundombinu kuongeza kasi ya kuifanyia matengenezo Mitambo yote ya Tume inayohitaji kutengenezwa ili iweze kutumika kibiashara na katika shughuli za ukarabati na ujenzi wa Miundombinu ya Umwagiliaji.
 
Ameishauri Idara hiyo kuboresha eneo la maegesho ya Mitambo pamoja na Stoo ya kuhifadhia vipuli vya Mashine wakati wa Matengenezo katika karakana ya Tume.
 
Mkuu wa kitengo cha ICT, GEOFREY MWAKIJUNGU (aliyekaa) akimwonyesha Mwenyekiti wa Bodi ya Tume Prof, Mahoo baadhi ya matukio katika Tovuti ya Tume.
Mwenyekiti wa Bodi Tume ya Taifa ya Umwagiliaji akikagua
Mtambo aina ya EXCAVATOR katika Ofisi za Tume Mkao Makuu Dodoma.

Post a Comment

Previous Post Next Post