WAZIRI BASHUNGWA AIPA BARAKA ZA MWISHO TAIFA QUEENS KATIKA MASHINDANO YA KOMBE LA NETIBOLI KWA NCHI ZA AFRIKA.

 Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa na Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa BMT Bi. Neema Msita wakiwa kwenye kikao pamoja na walimu, viongozi na wachezaji wa timu ya Taifa ya mchezo wa Netiboli (Taifa Queens) saa chache kabala ya kuwakabidhi bendera kuiwakilisha nchi katika mashindano ya kombe la Netiboli kwa nchi za Afrika yanayotarajiwa kufanyika nchini Namibia kuanzia Novemba 9, 2021.

Mwenyekiti wa Chama cha Netiboli Tanzania CHANETA Dkt. Devotha Marwa akizungumza wakati wa kikao baina ya Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa pamoja na walimu, viongozi na wachezaji wa timu ya Taifa ya mchezo wa Netiboli (Taifa Queens) saa chache kabala ya kuwakabidhi bendera kuiwakilisha nchi katika mashindano ya kombe la Netiboli kwa nchi za Afrika yanayotarajiwa kufanyika nchini Namibia kuanzia Novemba 9, 2021.

Baadhi ya wachezaji wa timu ya Taifa ya mchezo wa Netiboli (Taifa Queens) wakifurahia baada ya kukabidhiwa Bendera ya Tiafa na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa (Hayupo Pichani) kwa ajili ya kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya kombe la Netiboli kwa nchi za Afrika yanayotarajiwa kufanyika nchini Namibia kuanzia Novemba 9, 2021.

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa akimkabidhi bendera ya taifa kapteni wa timu ya Taifa ya mchezo wa Netiboli (Taifa Queens) Mwanahidi Ngubege kama ishara ya kuwatakia kila la kheri katika mashindano ya kombe la Netiboli kwa nchi za Afrika yanayotarajiwa kufanyika nchini Namibia kuanzia Novemba 9, 2021.

***************************

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa amewakabidhi Bendera ya Taifa, timu ya Taifa ya mchezo wa Netiboli (Taifa Queens) kama baraka na kheri katika mashindano ya kombe la Netiboli kwa nchi za Afrika yanayotarajiwa kufanyika nchini Namibia kuanzia Novemba 9, 2021.

Waziri Bashungwa amewakabidhi bendere hiyo leo Novemba 6, 2021 jijini Dar es Salaam akiwasisitiza kutambua dhamana waliyoibeba kwa niaba ya watanzania wote.

Waziri Bashunhgwsa amesema Serikali itaendelea kuwekeza nguvu, juhudi, maarifa na fedha katika kukuza kila aina ya michezo akiutaja mchezo wa netiboli kuwa ni miongoni mwa michezo sita iliyopewa kipaumbele na Wizara yake.

“Mkifanya vizuri huko hiyo ni furaha ya nchi, na mkifanya vibaya ni fedheha ya nchi, kwa maandalizi mliyoyafanya sisi kama taifa tunawaamini na tunaamini mtafanya vizuri, naomba niwaahidi kwamba siku mnaporejea hapa nchini mkiwa na kombe letu mikononi, nitakuja kuwapokea uwanja wa ndege kwa namna ya kipekee “ alisema waziri Bashungwa.

Awali akiongea na wachezaji wa timu hiyo Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Bi. Neema Msita amewataka wachezaji hao kuthamini hatua zilizochukuliwa na Serikali ikiwa ni pamoja na kutoa kiasi cha fedha, zaidi ya shilingi milioni 60 ili kugharamia usafiri na malazi ya wachezaji huko nchini Namibia.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Netiboli Tanzania (CHANETA) Dkt. Devotha Marwa ameipongeza Serikali kwa kutoa kiasi hicho cha fedha kuwezesha timu hiyo kushiriki katika mashindano hayo ya kimataifa akisema huo ni mwanzo mpya katika kuupaisha mchezo wa netiboli hapa nchini.

Timu ya Taifa ya mchezo wa Netiboli (Taifa Queens) inatarajiwa kuondoka nchini Novemba 7,  kuelekea nchini Namibia kushiriki mashindano ya kombe la Netiboli kwa nchi za Afrika ikiwa na matumaini kemkemu ya kuibuka bingwa katika mashindano hayo kutokana na maandalizi aliyoyafanya.

Post a Comment

Previous Post Next Post