WAZIRI MBARAWA ATOA MIEZI MINNE MKANDARASI KUKAMILISHA BARABARA

 


 

Na Mwandishiwetu ,Michuzi Tv Tanga

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa ametoa miezi minne kwa Mkandarasi wa Mradi wa Barabara ya Tanga-Pangani mkoani Tanga, kukamilisha ujenzi wa barabara hiyo.

Waziri Mbarawa ambaye yuko mkoani hapa kwa ziara ya siku mbili ya kikazi ameongozana na mwenyeji wake Mkuu wa Mkoa wa Tanga ambapo wametembelea Barabara ya Tanga-Pangani yenye urefu Km 50 na Muheza-Amani yenye Km 40.

"Nitakaporudi tena Februari mwaka 2022, nataka nione kazi zote zimemalizika na tuone lami hapa, wananchi wanataka kuona lami kwa hiyo niwaombe wenzangu na Mkuu wa Mkoa yuko hapa saa zote atapata fursa ya kuja kulisimamia tuhakikishe kwa oinamalizika ndani ya muda huo," amesema.

Kwa upande wake Malima amesema mradi huo una umuhimu wa kipekee kwa Mkoa wa Tanga hasa kwenye kufungua utalii wa Kanda ya Ufukwe wa Bahari na Hifadhi ya Saadani.

Post a Comment

Previous Post Next Post