VIONGOZI WA SKIMU ZA UMWAGILIAJI WATAKIWA KUSIMAMIA UKUSANYAJI WA ADA NA TOZO

 

Mhandisi Umwagiliaji Mkoa wa Iringa Bw. Onesmo Kahoggo akingumza kuhusu
Viongozi wa skimu za kilimo cha Umwagiliaji Nchini, kusimamia ukusanyaji
wa ada na Tozo za Umwagiliaji.
Bi Katarina Rashid Mlaga, mkulima mkazi wa kijiji cha Mgozi akiishuru
Serikali kwa kurejesha mto Ruaha Mdogo katika njia yake ya asili.
Picha Ikionesha mto Ruaha mdogo baada ya kurejeshwa katika njia yake ya asili.

Picha ikionesha Roli la kubebea mchanga likiwa kazini wakati wa ukarabati wa mto Ruaha mdogo.

Na; Mwandishi Wetu –
Pawaga Iringa.

Mhandisi wa Umwagiliaji Mkoa wa Iringa Onesmo Kahoggo amewataka viongozi katika Skimu za Umwagiliaji  kusimamia kikamilifu zoezi la ukusanyaji ada
na tozo  kwa lengo la kutunisha mfuko wa
Umwagiliaji.

Akizungumza mjini Iringa Bw, Kahoggo amesema endapo wakulima
katika Skimu za Umwagiliaji watachangia fedha za ada ya usajili na matunzo kwa
wakati, itasaidia kuharakisha ukarabati wa Skimu zilizoharibika kutokana na
athari zitokanazo na madhara ya mabadiliko ya tabia nchi pamoja na kujenga
Skimu mpya nchini.

Ametolea mfano zoezi la kuurejesha mto Ruaha Mdogo katika
njia yake ya asili limegharimu fedha kutoka mfuko wa Umwagiliaji ambao
unahitaji kuwezeshwa na wakulima hao.

Kwa upande wake Bi, Katarina Rashidi Mlaga  mkulima mkazi wa
kijiji cha Magozi ameishukuru serikali kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kwa
kazi kubwa iliyofanya wa kurejesha mto Ruaha Mdogo katika njia yake ya asili,
nakusema kuwa wakulima katika kijiji hicho hutegemea Zaidi kilimo cha
umwagiliaji, na wamepata elimu ya kutosha kuhusu uchangiaji wa tozo za
umwagiliaji na wapo tayari kuchangia.

Awali akiongea kijijini hapo Diwani wa kata ya Ilolo Mpya  Bw,
Funda Mihayo  amemshukuru Mkurugenzi wa
Tume ya taifa ya Umwagiliaji Bw, Daudi Kaali kwa kuwezesha wataalam wa tume
kurekebisha miundombinu ya mifereji ya kupeleka maji katika mashamba ya
wakulima pamoja na zoezi la usanifu linaloendelea katika Skimu ya Liganga
ambapo lengo ni kuwezesha maji kunyweshea Skimu ya Magozi na Mkombilenga.

Post a Comment

Previous Post Next Post