Madaktari wazawa wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa mara ya kwanza wakipandikiza mishipa miwili ya damu katika moyo bila ya kuusimamisha moyo (Off-Pump Coronary Artery Bypass Surgery) kwa mgonjwa ambaye mishipa yake mitatu ya damu ilikua imeziba na uwezo wa moyo kufanya kazi ukiwa umeshuka na kubaki asilimia 27 hivyo kumsababishia kuchoka na kushindwa kufanya kazi leo katika Taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam