MENEJA wa Kituo cha Uwekezaji Kanda ya Kati (TIC) Abubakari Ndwata,akizungumza leo June 3,2021 jijini Dodoma na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea eneo la uwekezaji wa Viwanda ambapo kunatarajiwa kujengwa kiwanda kikubwa cha mbolea kutoka kampuni ya Itra Com Kutoka Burundi.
Mwekezaji kutoka kampuni ya Itra Com Musafiri Dieudonne,akizungumza leo June 3,2021 jijini Dodoma na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea eneo la uwekezaji wa Viwanda ambapo kunatarajiwa kujengwa kiwanda kikubwa cha mbolea kutoka kampuni ya Itra Com Kutoka Burundi.
Mhandisi wa Mradi huo Tumaini Chonya kutoka Shirika la umeme TANESCO Dodoma,akizungumza leo June 3,2021 jijini Dodoma na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea eneo la uwekezaji wa Viwanda ambapo kunatarajiwa kujengwa kiwanda kikubwa cha mbolea kutoka kampuni ya Itra Com Kutoka Burundi.
Mafundi wakiendelea na kufunga nyaya za umeme katika eneo la Nala lililopo jijini Dodoma.
Mafundi wakichimba kisima cha Maji katika eneo la Nala lililopo jijini Dodoma.
Mafundi wakiendelea na kuchimba msingi kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda cha Mbolea eneo la Nala.
…………………………………………………………………
Na.Alex Sonna,Dodoma
MENEJA wa Kituo cha Uwekezaji Kanda ya Kati (TIC) Abubakari Ndwata amewataka wawekezaji kwenda kuwekeza katika eneo la Nala kwani tayari miundombinu ya umeme na maji tayari vinapatikana muda wote.
Kauli hiyo ameitoa leo June 3,2021 jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea eneo la uwekezaji wa Viwanda ambapo kunatarajiwa kujengwa kiwanda kikubwa cha mbolea kutoka kampuni ya Itra Com Kutoka Burundi.
Bw.Ndwata amesema kuwa zamani walikuwa wakija na muwekezaji kumuonesha eneo anaanza kujiuliza mbona miundombinu hakuna itakuwaje sasa hapa naweza kuwa na kiwanda kweli.
“Wapo wawekezaji ambao wamepata maeneo yao Nala ni muda muafaka sasa waje kwani ile shida ya umeme imeisha hivyo watu waje nala na visima vya maji vinaendelea kuchimbwa”amesema Ndwata.
Amesema kiwanda hicho ni kikubwa na kitakuwa na uwezo wa kutoa tani laki 500’000 za mbolea kwa mwaka.
“Kama tunavyojua tunaagiza mbolea nje karibu tani laki 700,000 hivyo kiwanda hiki katika eneo la Nala kitakuja kuokoa pesa zetu hapa Nchini”amesema Ndwata
“Rais Samia Suluhu Hassan amekuwa akisisitiza serikali na taasisi zake kuboresha huduma za uwekezaji,nawashukuru Tanesco kwa kuweza kutoa ushirikiano wa kutosha ambapo wameitikia na kufanya kazi kwa haraka ili muwekezaji aweze kuja kuanza kazi ya kujenga kiwanda hicho.
Aidha amewashukuru Duwasa kwa ushirikiano wao kwa kuanza kujenga kisima chenye lita 5000 mpaka 7000 za maji zinachimbwa na tunatarajia kuchimbwa kwa visima vitatu vya maji.
” Nawashukuru watoa huduma wa serikali ambao wamewezesha kama tulivyoona nguzo zimetandazwa kilometa Tano kutoka chanzo Cha umeme lakini Shirika la umeme Tanzania limewezesha kuhakikisha umeme umefika”amesema Ndwata
Sambamba na hayo ametoa wito kwa wawekezaji wengine ambao wana maeneo Nala kwenda kuanzisha viwanda kwani umeme na Maji yanapatikana muda wote
Kwa upande wake Mhandisi wa Mradi huo Tumaini Chonya kutoka Shirika la umeme TANESCO Dodoma amesema mradi huo upo katika hatua ya Mwisho ya kukamilisha ambapo transformer yenye ukubwa wa KVA 500 na nyingine KVA 50 imepita kwenye maeneo ya wananchi ili waweze kupata umeme.
“Muda sio mrefu laini zote zitakuwa na umeme hapa naweza kusema asilimia 95 za umeme zimekamilika na hadi kufikia kesho kutwa umeme utakuwa umewaka kwa asilimia 100 “amesema Mhandisi Chonya
Hata hivyo Mhandisi Chonya amesema kuwa wanamsubili muwekezaji aweze kuweka pointi zake za eneo la kuweka taa ili eneo liwe jeupe kwani leo umeme utawaka.
Naye Mwekezaji kutoka kampuni ya Itra Com Musafiri Dieudonne amesema kuwa anaishukuru serikali pamoja na TIC kwa kuweza kufanikisha eneo hilo kuwa na umeme pamoja na maji kwani ndio ilikuwa changamoto kubwa kwao.
Kasi imeonekana na Sisi itracom yunaahidi kuanzia wiki ijayo tutakuwa tumeanza mradi wetu wa Ujenzi wa kampuni ya mbolea lakini pia yunaahidi kuanzisha miradi mingine Mingi”amesema Deudonne
Naye Mhandisi wa Mradi kutoka Tanesco jijini Dodoma Tumaini Chonya alisema kuwa walipewa kazi ya kepeleka umeme nala ili waweze kulisha kiwanda cha muwekezaji hivyo laini hiyo kutokea barabarani ni km 5 na inamashine umba mbili.
“Lakini pia tuliona siyo vyema kuleta umeme kiwandani bila kuwapatia wananchi wa Nala wakakosa umeme hivyo nao tumepataia transfoma moja ya 50 KVA ambayo itawalisha wananchi na kuwapatia huduma ya umeme”
Zoezi hili limechukua siku saba ujenzi wa laini yote kutokea barabara kuu umbali wa km tano ,hivyo mafundi wa Tanesco wamefanya kazi usiku na mchana ilikuhakikisha kazi hii inakamilika haraka iwezekanavyo