WAZIRI NDALICHAKO AFUNGUA MAFUNZO RASMI KWA MAAFISA ELIMU WA MIKOA AWATAKA KUACHANA NA UDANG’ANYIFU

 

WAZIRI wa elimu sayansi  na teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akizungumza na maafisa elimu Mkoa, maaafisa elimu taaluma Mkoa pamoja na maafisa elimu msingi wa halmashauri mbali mbali wakati wa ufunguzi rasmi wa mafunzo ya uthibiti ubora wa elimu yaliyofanyika katika ukumbi wa Adem Wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.

Afisa mtendaji mkuu wa wakala wa maendeleo ya uongozi wa elimu (ADEM)  Dr. Siston Mgullah akisoma taarifa kwa mgeni rasmi kuhusiana na mafunzo hayo ambayo yameandaliwa maalumu kwa ajili ya kuweza kuwajengea uwezo maafisa elimu hao.

Baadhi ya washiriki mbali mbali ambao ni maafisa elimu Mkoa, maafisa elimu taaaluma Mkoa pamoja na maafisa elimu msingi kutoka halmashauri mbali mbali wakiwa katika ukumbi wa Adem kwa ajili ya kumsikiliza Waziri wa elimu sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako.

Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Zainabu Kawawa akitoa salamu zake kwa mgeni rasmi pamoja na kuzungumza na washiriki wa mafunzo hayo.

Afisa elimu wa Mkoa wa Dar es Salaam Halhaji Abdul Maulid wa kushoto akiwa na maafisa wenzake kutoka mikoa mbali mbali wakiwa wanapiga makofi kwa furaha  wakati walipokuwa wakimsikiliza Waziri wa elimu sayansi na teknolojia wakati wa mafunzo hayo.

………………………………………………………………..

NA VICTOR MASANGU, BAGAMOYO

WAZIRI wa elimu sayansi  na teknolojia Profesa Joyce Ndalichako amechukizwa na kukemea vikali vitendo vya baadhi ya maafisa elimu wa Mikoa na Wilaya kuwa na tabia ya kufanya  udanganyifu sababu ambayo inapelekea hali ya sintofahamu kwa wadau elimu  wa Tanzania na kuwataka kubadilika na kusimamia ipasavyo sera  pamoja na mitaala iliyopo kwa lengo la kuweza kukuza sekta ya elimu na kuzitafutia ufumbuzi changamoto zilizopo.

Ndalichako ametoa kauli hiyo wakati wa ufunguzi rami wa mafunzo maalumu ya siku nne  ya uthibiti ubora  wa ndani kwa kwa maafisa elimu wote wa Mikoa 26,maafisa elimu  wa taaluma wa Mkoa pamoja na maafisa elimu msingi kutoka halmashauri mbali mbali yaliyofanyika katika ukumbi wa  wakala wa maendeleo ya uongozi wa elimu (ADEM) Wilayani Bagamoyo Mkoa wa Pwani.

Pia aliwaagiza maafisa elimu hao kuweka mipango madhubuti katika sualazima la kusimamia fedha  za umma zinazotolewa na serikali katia kutekeleza miradi mbali mbali iliyopo katika sekta ya elimu na kwamba lengo la serikali ni kuhakikisha kwamba inaweka mazingira mazuri ya wanafunzi na kuboresha elimu katika ngazi zote.

“Kuna maagizo ambayo tayari yametolew na Rais wetu wa awamu ya sita wakati analihutubia bunge kwa hivyo hili ni agizo kwa kwamba yale yote ambayo yamesema inatakiwa tufafanyie kazi ipasavyo na sio mpaka msubilie mimi niwape taarifa na hili ni kwa lengo la kuweza kuleta mabadikilo chanya katia sekta yetu ya elimu na kwamba haya mafunzo myatumia vema uko mnapokwenda na  mimi ninawashukuru sana uongozi wa Adem katika kusimamia vema suala la elimu,alisema Ndalichako.

Awali  Afisa mtendaji mkuu wa wakala wa maendeleo ya uongozi wa elimu (ADEM)  Dr. Siston Mgullah akisoma taarifa kwa mgeni rasmi kuhusiana na mafunzo hayo ambapo amesema yamewashirikisha maafisa elimu Mkoa, maafisa elimu taalamu Mkoa pamoja na maafisa elimu msingi katika halmashauri mbali mbali kwa  lengo la kuwajengea uwezo na kuwapa  ujuzi katika suala zima la kusimamia uthibiti ubora wa elimu.

Dr. Mgullah aliongeza kuwa mafunzo hayo ambayo yatafanyika kwa kipindi cha muda wa siku nne lengo lake kubwa ni kuwajengea umahiri zaidi katika kuboresha  elimu sambamba na kuhakikisha wanawajibika ipasavyo katika kuchapa kazi kwa bidii lengo ikiwa ni kutimiza malengo ya kukuza sekta ya elimu hapa nchini.

“Napenda kuchukua fursa hii kuwashukuru washiriki wote wa mafunzo haya pamoja na kuwashukuru wakufunzi mbali mbali wa Wakala wa ADEM kwa maandaliziambayo wameyafanya katika kutimiza jambo hili pamoja na Waziri wa elimu kuja kwa ajili ya kutufungulia rasmi mafunzo haya  katika mafunzo haya,”alisema. Mgullah.

Halhaji Abdul Maulid ambaye ni Afisa elimu wa Mkoa wa Dar es  Salaam  amebainisha kwamba kufanyika kwa mafunzo hayo ya uthibiti ubora kutaweza kuwa mkombozi mkubwa katika kuleta mabadiliko chanya katika kuongeza zaidi kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi sambamba na  uwajibikaji na ujuzi katika kuboresha sekta ya elimu.

Pia Afisa elimu huyo alifafanua kwamba baada ya kumalizika mafunzo hayo yataweza kuwapa fursa ya kubadilishana uzoefu na maafisa elimu wengine kutoka mikoa mbali mbali na kwamba atahakikisha anaweka mipango imara na madhiubuti katika kusimamia ipasavyo maelekezo yote amabyo yametolewa na waziri wa elimu kwa kuyafanyia kazi kwa vitendo.

“Kwanza sisi kama wasimamizi wa elimu na mimi kama Afisa elimu wa Mkoa wa Dar es Salaam tunaishukuru serikali pamoja na Adem kwa kuweza kutukutanisha kwa pamoja maafisa elimu wa mikoa yote ya Tanzania, maafisa elimu wanaosimamia elimu ya msingi pamoja na wataalamu wengine hii maana yake sasa tunashirikiana kwa pamoja ili kuweza kuleta mageuzi katika sualala uhibiti ubora wa elimu na nina imani tutafanikiwa,’alifafanua Maulid.

Kwa upande wake Afisa elimu wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe Shomari Bane ambaye anasimamia elimu ya msingi amesema kuwa mafunzo hayo yataweza kuwajengea uwezo mkubwa katika  suala zima la kutekeleza wajibu wao ipasavyo na kwamba yataweza kuwaongezea ujuzi na umahiri katika kutoa huduma ya elimu inavyotakiwa kwa wanafunzi.

Pia Afisa huyo alisema kwamba baada ya mafunzo hayo yataweza kwenda kuleta mabadiliko chanya katika suala zima la uthibiti ubora wa elimu, pamoja na kusimamia ipasavyo jinsi ya mwenendo mzima wa mitaala ya elimu inayotumika kwa sasa lengo na kuahidi kuyafanyia kazi maagizo yote ambayo yametolewa na Waziri wa elimu.

Naye Mkuu wa Wilaya ya ya Bagamoyo Zainabu Kawawa amewahasa walimu hao wakuu kutumia fursa waliyoipata kwa kuhakikisha wanatembelea vivutia mbali mbali vya utalii na makumbusho yaliyopo kwa lengo la kujifunza mambo mabli mbali ya kihistoria  ambayo yataweza kuwasaidia pindi wanapofundisha somo la historia.

Post a Comment

Previous Post Next Post