TBS YATOA WITO KWA WANANCHI KUTUMIA BIDHAA ZILIZOTHIBITISHWA UBORA WAKE

 

Afisa Masoko wa TBS, Rhoda Mayugu akimhudumia mmoja wa watu
waliohudhuria kwenye banda lao katika maonyesho hayo ya Wiki ya Maziwa
mjini Tanga

Afisa Udhibiti wa TBS, Emmanuel Bashakaya akimhudumia mmoja wa wadau wa maonyesho ya  wiki ya maziwa yaliyofanyika mjini Tanga

NA OSCAR  ASSENGA,TANGA
SHIRIKA
la Viwango Tanzania (TBS), limewaasa wananchi kutumia bidhaa
zilizothibitishwa ubora wake ili kuweza kuepukana na athari mbalimbali
wanazoweze kukutana nazo kutokana na kununua zile ambazo
hazijathibitishwa
Afisa
Masoko wa TBS, Rhoda Mayugu alisema hayo katika maonyesho ya Wiki ya
Maziwa yanayoendelea kwenye viwanja vya Tangamano Jijini Tanga. 
Rhoda anasema kuna umuhimu mkubwa kwa wananchi kutumia bidhaa zilizothibitishwa ubora wake.
“Tumetumia maonyesho haya kutoa elimu kwa wananchi kuhusu faida ya kutumia bidhaa zilizothibitishwa ubora wake,” asema Rhoda.
Akizungumzia
maonyesho hayo yaliyoanza tangu Mei 31, mwaka huu na yanatarajiwa
kufungwa leo, Rhoda amesema lengo kushiriki lilikuwa kuwafikia wadau wa
maziwa na kuwapatia elimu kuhusu umuhimu na faida ya kuthibitisha ubora
wa bidhaa zao.
 Rhoda anasema wamefurahishwa na mwitikio wa wahudhuriaji wa maonyesho hayo na utayari wa kuthibitisha ubora wa bidhaa zao.
“Tumefurahishwa
na mwitikio wa wengi waliohudhuria maonyesho hayo kuwa tayari
kuthibitisha ubora wa bidhaa zao na hata wale ambao hawajathibitisha
wako kwenye mchakato wa kufanya hivyo,” alisema Rhoda.

Post a Comment

Previous Post Next Post