TIC YAKAA NA WADAU WA MBOLEA KUJADILI KUHUSU UJENZI WA KIWANDA CHA MBOLEA CHA MWEKEZAJI ALIKO DANGOTE

   Mkurugenzi Mtendaji wa TIC, Bw.Maduhu Kazi akizungumza katika kikao na watumishi wa wizara na taasisi mbalimbali baada ya kuitikia wito wa Muwekezaji nchini  Aliko Dangote kuwekeza kiwanda cha mbolea hapa nchini. Kikao hicho kimefanyika leo Makao Makuu ya Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Jijini Dar es Salaam.   

Wakuu wa taasisi mbalimbali wakiwa katika kikao hicho.

PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO

************************

NA EMMANUEL MBATILO

Kituo cha uwekezaji nchini TIC, kimekutana na wadau wa mbolea nchini pamoja na viongozi wa manspaa ya kilwa ili kujadili kwa pamoja juu ya ujenzi wa kiwanda kikubwa cha mbolea cha muwekezaji Alhaj Aliko Dangote hapa nchini.

Akizungumza mara baada ya kikao hicho kilichofanyika leo Jijini Dar es Salaam Dar es salaam, Mkurugenzi wa mtendaji wa TIC, Mhe.Maduhu Kazi amesema kuwa wamekutana kwa pamoja ili kujadili ufanikishaji wa ombi la mwekezaji huyo mara baada yakuonesha nia ya kujenga kiwanda cha mbolea wakati alipofika nchini na kuzungumza na Rais Samia Suluhu Hassani.

“Tayari mazingira na eneo lipo tayari kwa mwekezaji huyo kwa ajili ya uwekezaji ikiwemo miundombinu wezeshi kujengwa katika kiwanda hicho”. Amesema Mhe.Kazi.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manspaa ya Kilwa Bw.Renatus Mchau amesema wapo tayari kumpatia eneo bure mwekezaji wa ujenzi wa kiwanda hicho ili aweze kuwekeza nhini na kuwezesha vijana wakitanzania kupata ajira.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA), Bw.Stephan Ngailo amesema asimia 90 ya mbolea inayotumika hapa nchini inatoka nje ya nchi hivyo uwepo wa kiwanda hicho utasaidia kuokoa fedha nyingi kwenda nje ya nchi.

Post a Comment

Previous Post Next Post