COSTECH YAWANOA WANAWAKE JUU YA SAYANSI NA TEKNOLOJIA

 

Washiriki wanawake wa mdahalo wa  Sayansi na Teknolojia kutoka vyuo mbali mbali nchini wakiwemo chuo cha Ustawi wa Jamii wakiwa katika picha ya pamoja kabla y kuanza kwa mdahalo huo.
Patience Abraham kutoka ukumbi wa Ubunifu wa Costech (Buni Innovation Hub) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ufunguzi wa mdahalo wa kujifunza matumizi ya Sayansi na Teknolojia kwa wanawake. Jijini Dar es Salaam.
Meneja Mipango, Ufuatiliaji na Tathmini wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Anna Ngoo, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ufunguzi wa mdahalo wa kujifunza matumizi ya Sayansi na Teknolojia kwa wanawake. Jijini Dar es Salaam.
Iku Mwanjisi kutoka Jukwaa Maalumu kwa ajili ya wanawake wenye mawazo ya kibunifu na ujasiliamali (Ndoto Hub) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ufunguzi wa mdahalo wa kujifunza matumizi ya Sayansi na Teknolojia kwa wanawake. Jijini Dar es Salaam.

WANAWAKE wameaswa kujituma na kujikita kwenye fani mbali mbali za Teknolojia na kuingia kwenye uongozi kwani hakuna jambo ambalo haliwezekani kufanyika na mwanamke. 

Patience Abraham kutoka kumbi ya Ubunifu ya Tume ya Sayansi na Teknolojia (Buni innovation Hub), ameyasema hayo leo Juni 29,2021 wakati wa mdahalo wa siku mbili juu ya masuala ya Sayansi na Teknolojia kwa wanawake.

Amesema dhumuni la mdahalo huo ni kuwahamasisha wanawake kujihusisha na masuala ya teknolojia ambayo itawasaidia katika mambo yao mbalimbali, kwa sababu wengi hawapo kwenye teknolojia.

"Katika mdahalo huu, kutakuwa na wadau kutoka sekta mbali mbali wakiwemo Vodacom, UNDP na Women in Technology ambapo kwa pamoja watajadili na kuhamasisha wanawake kujitambua katika masuala teknolojia na ubunifu.

"Wanawake wengine ni wabunifu lakini hawana elimu juu ya masuala ya Sayansi na Teknolojia, hivyo, Hub hii itawasaidia wanawake kujiingiza zaidi kwenye mambo ya Teknolojia sayansi, Ubunifu na Ujasiliamali amesema Patience.

Kwa upande wake, Meneja Mipango, Ufuatiliaji na Tathmini wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Anna Ngoo, amesema mdahalo huo utawasaidia wanawake vijana kuweza kujikita katika masuala ya Teknolojia katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku.  

Amesema Teknolojia itawarahisishia katika masuala yao mengi katika kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi na tija, kwa sababu hivi sasa teknolojia imekuwa kwa kiasi kikubwa.

"Naona wengi ni wanafunzi wa vyou, hili tamasha ambao unaambatana na mafunzo, utawasaidia kutambua umuhimu wa teknolojia na matumizi yake na pia itawafanya wawe wabunifu," alisema Ngowe.

Akizungumzia kuhusu uchumi na Teknolojia, Iku Mwanjisi kutoka Jukwaa Maalumu kwa ajili ya wanawake wenye mawazo ya kibunifu na ujasiliamali (Ndoto HUB), amesema katika kukuza uchumi au kuleta maendeleo, lazima mwanamke ashirikishwe.

"Mdahalo huu una lengo la kuwatambua wanawake katika sekta nzima ya Teknolojia nchini kwani hivi sasa, wanawake wanatakiwa wawe wabunifu na waendane na teknolojia iliyopo, Amesema.

Amesema mwanamke ni muhimu katika jamii na katika kukuza uchumi, hivyo kwao imekuwa ni muhimu kuwepo katika huo mdahalo ambapo watazungumza na wasichana wa vyuo mbali mbali na tunatarajia kwamba kutakuwa na mabadiliko makubwa na kuwachomoa wanawake zaidi waingie katika fani hii ya teknolojia haswa kwa ajili ya Maendeleo ya uchumi wa nchi yetu.

Mmoja wa wanufaika wa tamasha hilo, Subira Hamisi ambae ni mwanafunzi wa Chuo Cha Ustawi wa Jamii amesema, lengo la kuwepo katika tamasha hilo anataka  

kujifunza na kujua mambo tofauti tofauti kuhusiana na mwanamke, jinsi ya kuwezeshwa na pia anatarajia kujifunza zaidi namna ya kutumia teknolojia. 

" Natarajia kujifunza mambo mengi hasa masuala ya rasilimali watu na utawala, nikiwa kama mtoto wa kike natarajia kutimiza ndoto zangu, kwa sababu nataka kuwa mfanyabiashara mkubwa nchini na nje ya Tanzania, kwa hiyo tamasha hili litanisaidia kuhusiana na teknolojia."Alisema 

Post a Comment

Previous Post Next Post