WAZIRI NDUMBARO AWATOA HOFU WATUMISHI WA TTB

 

……………………………………………………..
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro amewatoa hofu  Watumishi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) kutokana na hofu iliyotanda miongoni  mwao na hivyo  kuwahimiza  kuendelea kuchapa kazi kama kawaida.

Hatua hiyo inakuja kufuatia kukabidhiwa taarifa ya Kamati iliyoundwa kuchunguza  tuhuma za ubadhirifu wa fedha pamoja matumizi mabaya ya Rasilimali Watu zinazoikabili TTB
Ametoa rai hiyo Jijini Dar es Salaam wakati alipokuwa akizungumza na Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya TTB mara baada ya  kupokea  taarifa ya Kamati ya uchunguzi wa tuhuma hizo.
 Waziri Dkt.Ndumbaro amesema hatua ya maamuzi ya taarifa hiyo yataanza kuchukuliwa  mwezi Juni mwaka huu kutokana na sasa kukabiliwa na majukumu mengine.
Amesema  mara tu baada ya kuipokea taarifa hiyo naye amemkabidhi Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt.Allan Kijazi kwa ajili ya kuifanyia kazi.
” Nakuagiza Mkurugenzi Mkuu wa TTB itisha kikao na  Watumishi zungumza nao watoe hofu wahimize waendelee kuchapa kazi kama kawaida, kama Wizara tutatoa maamuzi ya haki muda ukifika ” amesisitiza Dkt.Ndumbaro
Amesema majukumu ya msingi ya Bodi hiyo hayatakiwi yasimame yakisubiria hatua za maamuzi ya ripoti hiyo mpaka yatolewe.
Kufuatia hali hiyo, Waziri Dkt. Ndumbaro amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa TTB kumchukulia hatua Mtumishi yeyote ambaye hatatekeleza majukumu yake kwa visingizio vya  kusubilia  hadi pale  maamuzi ya ripoti yatakapotolewa.
Itakumbukwa mnamo tarehe 10 April, 2021 Waziri wa Maliasili na Utalii,Dkt.Damas Ndumbaro alimsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa TTB, DevothaMdachi ili kupisha uchunguzi wa tuhuma za  ubadhirifu wa fedha pamoja  na matumizi mabaya ya Rasilimali watu zinazoikabili Taasisi hiyo.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa TTB, Betrita Lyimo amesema atatekeleza maelekezo hayo ikiwemo kuitisha kikao cha Watumishi wote wa Taasisi hiyo kwa lengo la  kuzungumza nao kwa kuwatia moyo na kuwasisitiza Wachape ka

Post a Comment

Previous Post Next Post