WAZALISHAJI WA MAZIWA TANGA WAJIUNGA NA NHIF KWA KUWEZESHWA NA BENKI YA CRDB

Afisa
Mkuu wa Biashara wa Benki ya CRDB Dkt. Joseph Witts kushoto akiwa 
Mkurugenzi wa Huduma za Wanachama wa NHIF,Christopher Mapunda kulia wakisaini  makubaliano
na Wazalishaji wa Maziwa kupitia chama cha TDCU linaashiria utekelezaji wa
makubaliano ambayo Benki ya CRDB na NHIF  
wataweza kunufaika na mpango wa
Ushirika Afya unaoratibiwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya
Afya (NHIF) kwa kuwezeshwa kujiunga na Benki ya CRDB kupitia Chama cha
Ushirika
cha Wazalishaji wa Maziwa Tanga mjini (Tanga Diary Cooperative
Union(TDCU) kulia ni Meneja wa CRDB Kanda ya Kaskazini Chiku Issa halfa
ilifanyika Jijini Tanga

wataweza
kunufaika na mpango wa Ushirika Afya unaoratibiwa na Mfuko wa Taifa wa
Bima ya
Afya (NHIF) kwa kuwezeshwa kujiunga na Benki ya CRDB kupitia Chama cha
Ushirika
cha Wazalishaji wa Maziwa Tanga mjini (Tanga Diary Cooperative
Union(TDCU) kulia ni Meneja wa CRDB Kanda ya Kaskazini Chiku Issa halfa
ilifanyika Jijini Tanga

Afisa
Mkuu wa Biashara wa Benki ya CRDB Dkt. Joseph Witts kushoto akiwa 
Mkurugenzi wa Huduma za Wanachama wa NHIF,Christopher Mapunda kulia wakisaini  makubaliano
na Wazalishaji wa Maziwa kupitia chama cha TDCU linaashiria utekelezaji wa
makubaliano ambayo Benki ya CRDB na NHIF  
wataweza kunufaika na mpango wa
Ushirika Afya unaoratibiwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya
Afya (NHIF) kwa kuwezeshwa kujiunga na Benki ya CRDB kupitia Chama cha
Ushirika
cha Wazalishaji wa Maziwa Tanga mjini (Tanga Diary Cooperative
Union(TDCU) kulia ni Meneja wa CRDB Kanda ya Kaskazini Chiku Issa halfa
hiyo ilifanyika Jijini Tanga

Afisa
Mkuu wa Biashara wa Benki ya CRDB Dkt. Joseph Witts kulia
wakibadilishana hati za makubaliano na Mwenyekiti wa  TDCU Shamte Saudi
mara baada ya kuingia makubaliano hayo wanaoshuhudia ni Mkuu wa wilaya
ya Tanga Thobias Mwilapwa ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Tanga
Adam Malima na Mrajisi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Tanga Jackline
Senzighe

Afisa
Mkuu wa Biashara wa Benki ya CRDB Dkt. Joseph Witts kushoto akiwa 
Mkurugenzi wa Huduma za Wanachama wa NHIF,Christopher Mapunda kulia wakisaini  makubaliano
na Wazalishaji wa Maziwa kupitia chama cha TDCU linaashiria utekelezaji wa
makubaliano ambayo Benki ya CRDB na NHIF  
wataweza kunufaika na mpango wa
Ushirika Afya unaoratibiwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya
Afya (NHIF) kwa kuwezeshwa kujiunga na Benki ya CRDB kupitia Chama cha
Ushirika
cha Wazalishaji wa Maziwa Tanga mjini (Tanga Diary Cooperative
Union(TDCU) kulia ni Meneja wa CRDB Kanda ya Kaskazini Chiku Issa halfa
ilifanyika Jijini Tanga

Afisa
Mkuu wa Biashara wa Benki ya CRDB Dkt. Joseph Witts kushoto akiwa 
Mkurugenzi wa Huduma za Wanachama wa NHIF,Christopher Mapunda kulia wakisaini  makubaliano
na Wazalishaji wa Maziwa kupitia chama cha TDCU linaashiria utekelezaji wa
makubaliano ambayo Benki ya CRDB na NHIF  
wataweza kunufaika na mpango wa
Ushirika Afya unaoratibiwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya
Afya (NHIF) kwa kuwezeshwa kujiunga na Benki ya CRDB kupitia Chama cha
Ushirika
cha Wazalishaji wa Maziwa Tanga mjini (Tanga Diary Cooperative
Union(TDCU) kulia ni Meneja wa CRDB Kanda ya Kaskazini Chiku Issa halfa
iliyofanyika Jijini Tanga

Afisa
Mkuu wa Biashara wa Benki ya CRDB Dkt. Joseph Witts kulia
wakibadilishana hati za makubaliano na Mwenyekiti wa  TDCU Shamte Saudi
mara baada ya kuingia makubaliano hayo wanaoshuhudia ni Mkuu wa wilaya
ya Tanga Thobias Mwilapwa ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Tanga Adam Malima na Mrajisi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Tanga
Jackline Senzighe

WAZALISHAJI wa Maziwa Tanga mjini wataanza
kunufaika na mpango wa Ushirika Afya unaoratibiwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya
Afya (NHIF) kwa kuwezeshwa kujiunga na Benki ya CRDB kupitia Chama cha Ushirika
cha Wazalishaji wa Maziwa Tanga mjini (Tanga Diary Cooperative Union(TDCU).

Hatua hiyo inatokana na kuingia makubaliano
na Wazalishaji wa Maziwa kupitia chama cha TDCU linaashiria utekelezaji wa
makubaliano ambayo Benki ya CRDB na NHIF waliingia siku chache zilizopita za
kuwawezesha wana ushirika kujiunga na bima ya afya kwa utaratibu wa Ushirika
Afya.
 
Katika makubaliano hayo, Benki ya CRDB
itamlipia mwana ushirika michango ya bima ya afya kwa wakati na mwana ushirika
huyu atairejesha bila riba wakati wa msimu wa mauzo.
 
Akizungumza katika uzinduzi wa mpango
huo, Mkurugenzi wa Huduma za Wanachama wa NHIF,Christopher Mapunda amesema kuwa
ushirikiano huo na Benki ya CRDB ulianza tangu Mei 5, 2021 kwa pande zote mbili
kusaini Makubaliano ambayo yatawawezesha wanachama walio kwenye Vyama vya
Ushirika kunufaika na huduma za matibabu kupitia bima ya afya bila kuwa na
changamoto ya kifedha.

“Mfuko umeazimia kuwafikia watanzania
wote na huduma za Bima ya afya ili waweze kupata huduma za matibabu kwa urahisi
ndio maana tumekubaliana na Benki ya CRDB ambao ni wadau wakubwa wa wana
ushirika nchini kuwawezesha wana ushirika kujiunga na bima ya afya bila
changamoto ya kifedha”alisema Mapunda.

Akizungumzia huduma, Mapunda alisema
kuwa mwana ushirika na familia yake atapata huduma zote za matibabu katika
mtandao mpana wa vituo zaidi ya 8,000 Tanzania Bara na Zanzibar kuanzia ngazi
ya Zahanati hadi Hospitali ya Taifa.

Akizingumza katika tukio hilo, Afisa
Mkuu wa Biashara wa Benki ya CRDB Dkt. Joseph Witts amesema Benki ya CRDB iko
mstari wa mbele katika kuhudumia wana ushirika kwa namna mbalimbali na sasa
inamwezesha mwana ushirika kujiunga na bima ya afya kwa kulipia michango yake
kwa mwaka ili wakati wa mauzo ndipo airejeshe bila riba yoyote juu yake.

“Tunaungana na Serikali yetu katika
kuhakikisha wana ushirika nchini wanafanikiwa kwa kuwa na uhakika wa matibabu
na katika hili Benki ya CRDB tutamchangia mwana ushirika mchango wa bima ya
afya wa mwaka wa Shilingi 76,800 na mwenza wake kiwango hicho hicho na kwa kila
mtoto Shilingi 50,400 kwa mwaka.

Alisema nia yao ni kuunga mkono juhudi
za Serikali katika kuhakikisha Watanzania wote wanakuwa na bima ya afya kama
ambavyo Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan amekuwa akisisitiza na tumeanza na kundi
la wana ushirika kwa sababu ndio sekta inayoajiri watu wengi zaidi nchini”
alisema Dkt. Witts.

Akizungumzia huduma za Benki ya CRDB
alisema Wana ushirika hawata pata shida ya huduma za kibenki kwa kuwa ina
mtandao mpana wa matawi 246, wakala zaidi ya 19,000 na ATM 550 nchi nzima hivyo
ni rahisi kwao na wananchi wengine kupata huduma kwa karibu zaidi.

Mpango huu unazinduliwa kwa Wazalishaji wa Maziwa
Tanga mjini ukiwa ni mwendelezo wa kuwafikia wana ushirika wote nchini hivyo
wanachama kupitia Vyama vyao vya Ushirika wanahimizwa kujiunga kwa kuwa ni wa
manufaa, hauna riba yeyote kwa mkulima na wanarejesha michango ya bima ya afya
baada ya mauzo ya bidhaa husika.

Tangu kuanza kwa ushirikiano
huu baina ya NHIF na Benki ya CRDB Mei 5, 2021, vyama vya 
Chunya
Tobacco-growers Cooperative Union (CHUTCU), Maziwa Cooperative Union (MCU),
Muungano wa Wauza Maziwa wa Rungwe (MWAMARU) na Tanga Diary Cooperative Union (TDCU) vimeshaanza
kunufaika na tunategemea vyama vingi zaidi kujiunga na kunufaika na mpango huu.

Awali akizungumza wakati tukio la kutiliana saina
kwa ajili ya kutekeleza makubaliano Mkuu wa
wilaya ya
Tanga Thobias Mwilapwa ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Tanga Adam
Malima alisema hilo ni jambo nzuri na lenye tija kubwa kwa kwa manufaa
zaidi ya wazalishaji wa maziwa mkoani humo

DC Mwilapwa Benki ya CRDB na NHIF kwa
jinsi walivyokuja na mpamgo huo utasaidia kuleta  manufaa makubwa kwa wananchi kutokana na
kwamba dira ya Taifa ya maendeleo 2020/2025 inaeleza kwamba itakapofika 2025
watanzania wote wawe wameingia kwenye mpango utakaowahakikishia wanaweza kupata
huduma ya afya wakati wowote bila kujali vipato vyao.

“Wakati huo utakapofika kwenye lengo
hilo namna peke yake kuhakikisha watanzania wanapata tiba bila kupitia vipato
vyao ni kupitia huduma ya afya hivyo ni wazo jema kutekeleza azma ya serikali
lakini kutekeleza mambo makubwa lazima uwe na uwez,i rasiliamali fedha”Alisema

Mkuu huyo wa wilaya aliwapongeza kwa
mpango huo ambao alisema unaitoa kimasomaso Serikali watanzania ni jambo jema
watokee watu ambao wanakubaliana nalo nao ni Benki ya CRDB ambao wamesaidia
kuwezesha kwenye uwezeshaji wa kifedha.

 “Mmewezsha
mkopo usio na riba mnapofanya hilo hamtekelezi lile la 2020/2025 ambalo ni la
Tanzania lakini mnatekeleza malengo ya maendeleo endelevu ambavyo yanafikia
mwaka 2030 wenzetu umoja wa mataifa wanafikiria dunia watu wote wawe wameingia
kwenye mpango wa bima ya afya lakini sisi tunasema kabla ya wengine wote
duniani hawajafikia tutakuwa tumefika 2025”Alisema DC Mwilapwa.

Alisisitiza kwamba Mfuko wa Bima ya
Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) wamefanya kazi yao kutekeleza agizo la serikali na
CRDB wanafanya kazi kusaidia jitihada za mfuko huo lakini jambo jingine
mliloliangalia ili unufaike lazima uwe mwana ushiriki hivyo watakwenda kuona
maendeleo makubwa kwenye ushiriki kwa kupatiwa bima ya afya,

Naye kwa upande wake Mrajis wa vyama vya
Ushiriki mkoa wa Tanga Jacquiline Senzighe
alitoa shukruani kwa mwelekeo uliopo mbele yao wa kuwa na bima ya afya
kwa wafugaji lakini mpango huo unategemewa kwenye ushiriki wote na hizo ni
habari njema zenye manufaa makubwa kwao.

Alisema kwa sababu wanaushirika lazima
watoke ili waweze kutoka wanapaswa kuwa na afya njema huku akieleza kwa sasa mkoa
wa Tanga inafanyika kwa kuanzia vyama vya ushirika vya wafugaji ambao vikifanya
vizuri zaidi vitasaidia vyama vyengine kufikika kwa urahisi zaidi.

“Lakini nitoe wito kwa vyama vya
ushirika na viongozi mliopata mkopo lakini lazima mtambue kwamba marejesho yake
ni kupitia zile shughuli ambazo wanaushirika wanazifanya kila siku ”Alisisitiza
.

Mrajisi huyo alisema iwapo mkopo huo
ukiendelea vizuri na wakiendelea kufanya ushirikiano mzuri wataendelea kufungua
wigo mpana kwa vyama vyengine vya ushirika vya mchepuo mwengine kuweza kunufaika
nao.

Hata hivyo kwa upande wake Katibu
Mtendaji wa Chama cha Ushirika cha Wazalishaji wa Maziwa Tanga mjini (Tanga
Diary Cooperative Union (TDCU) Athumani Mahadhi alisema chama hicho
kilianzishwa mwaka 1993 wakiwa na lengo la kutafuta soko la wafugaji wa Ng’ombe
wa maziwa mkoa wa Tanga.

Alisema kwea sasa wana vyama wanachama
28 na wafugaji mmoja mmoja wamefikia kwa mkoa mzima wamefikia 6285 huku
akieleza katika mpango huo wa bima ya afya wao kama TDCU na vyama vya  wanaona kama itakuwa itachochea baadhi ya
watu ambao sio wanachma  kuona ipo haja
ya kujiunga kwenye vyama vya ushirika kutokana na kwamba huduma ya afya pia
inapatikana huko.

Post a Comment

Previous Post Next Post