MAMADOU SAKHO AKUBALI KUWA BALOZI WA HIYARI WA UTALII WA TANZANIA.

  Mchezaji wa timu ya mpira wa miguu wa Kilabu ya Crystal Palace inayoshiriki ligi kuu ya Uingereza (EPL) na Mchezaji wa timu ya taifa ya Ufaransa amekubali ombi la Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) kuwa Balozi wa Hiyari wa Utalii wa Tanzania. Mamadou amekubali ombi hili wakati alipokutana na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TTB, Betrita Lyimo katika Hifadhi ya Bonde la Ngorongoro.


Mamadou ambaye ni raia wa Ufaransa amewasili nchini Tanzania tarehe 26/5/2021 kwa mapumziko ya siku 10 akiwa ameambatana na familia yake wametembelea vivutio vya utalii vya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, Kijiji cha Wamasai cha Seneto, Hifadhi ya Bonde la Ngorongoro na Visiwa vya Zanzibar.

Aidha, Timu ya Waandishi wa habari wa Televishen ya TF1 ya nchini Ufaransa imewalisili nchini Tanzania tarehe 27/5/2021 kwa lengo la kutengeneza makala maalumu ya ziara ya Mamadou itakayotumika kutangaza utalii wa Tanzania kwenye soko la utalii la Ufaransa hususani maeneo yote ya vivutio vya utalii aliyotembelea mchezaji huyu Maarufu.

Tanzania inaendelea inapokea wanamichezo kutoka nchi mbalimbali duniani wanaokuja na familia zao kutembelea vivutio vya utalii vya Tanzania. Hii ni fursa adhimu kwa TTB kuendelea kushirikiana na wanamichezo kutangaza utalii wa Tanzania hasa wenye wafuasi wengi kwenye mitandao yao ya kijamii ambayo ni nyenzo muhimu yenye kufikifiksha ujumbe kwa watu wengi ndani ya muda mfupi. kwa ziara ya matembezi ya siku 10. Mchezaji huyu


Mchezaji Mamadou Sakho na familia yake wakiangalia burudani ya ngoma ya Kimasai wakati alipotembelea kijiji cha Wamasai wanaoishi katika Hifadhi ya Bonde la Ngorongoro.
 

Mchezaji mpira wa Miguu Mamadou Sakho na familia yake wakionyesha vyeti walivyopata baada ya kumaliza safari yao ya utalii wa kutumia puto (Balloon Safari) katika Hifadhi ya Bonde la Ngorongoro.
Mchezaji mpira wa Miguu Mamadou Sakho akiwa na familia yake katika hifadhi ya Bonde la Ngorongoro.

Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii (TTB) Betrita Lyimo akiwa pamoja na Mamadou Sakho, Mchezaji wa mpira wa miguu kilabu ya Crystal Palace inayoshiriki ligi kuu ya Uingereza (EPL) na mchezaji wa timu ya Taifa ya Ufaransa.

Post a Comment

Previous Post Next Post