WASHINDI 10 WA INSHA KUKABIDHIWA ZAWADI SIKU YA VIWANGO AFRIKA

   

Afisa Viwango TBS, Bw.Henry Msuya akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Shirika la Viwango Tanzania (TBS).

************************************

NA EMMANUEL MBATILO,DAR ES SALAAM

Kuelekea maadhimisho ya Siku ya Viwango Afrika yatakayofanyika Mei 6 mwaka huu, Shirika la Viwango Tanzania limeandaa zawadi kwa Wanafunzi 10 waliofanya vizuri katika uandishi wa Insha ambapo mashindano hayo yalifanyika hivi karibuni katika Vyuo Vikuu na Vyuo vya Kati hapa nchini.

Akizungumza na mwandishi wetu leo Jijini Dar es Salaam, Afisa Viwango TBS, Bw.Henry Msuya amesema kuwa katika shindano hilo la Insha Mada Kuu ilikuwa ni UMUHIMU WA VIWANGO KATIKA KUKUZA SANAA,UTAMADUNI NA TURATHI likiwa lengo kuwasaidia wanafunzi wajue kwenye sekta husika ni nini kinahitajika katika kukidhi viwango.

“Tutawapa zawadi wanafunzi 10 walioshinda shindano hilo pia watapelekwa kushiriki shindano la Afrika nzima kumpata mshindi wa Afrika”.

Aidha Bw.Msuya amesema kuwa shindano hilo liliandaliwa na Shirika la Viwango Afrikab(ARSO) ambapo TBS wao walikuwa na jukumu la kusimamia hapa nchini.

“Ushiriki umekuwa mkubwa tumepata zaidi ya wanafunzi 214 walioshiriki shindano hilo kutoka Vyuo Vikuu na Vyuo vya Kati 32 hapa nchini”. Amesema Bw.Msuya.

Post a Comment

Previous Post Next Post