TBS YAENDESHA MAFUNZO KWA WAJASILIAMALI KUHUSU VIWANGO MKOANI MOROGORO

   

************************************

Shirika la Viwango Tanzania limetoa mafunzo kwa wajasiliamali na wafanyabiashara mkoani Morogoro ambaoi limewataka kuendelea kuzalisha bidhaa zinazokidhi viwango ili kuweza kumlinda mtumiaji.

Akizungumza katika mafunzo hayo Meneja wa Mafunzo na Utafiti TBS, Mwl.Hamisi Mwanasala amesema kuwa wajasiliamali wanachangia kwa kiasi kikubwa katika kukuza uchumi wa nchi hivyo wameona ni vyema kuwapa mafunzo ili kuhakikisha wanazalisha na kuuza bidhaa zilizokidhi viwango.

“Ili tuendelee kukuza biashara zetu tunatakiwa kuzalisha bidhaa zenye ubora unaokubalika na tuweze kuingia katika soko la ushindani na tuendele kuwa kwenye soko liwe la ndani ama la nje”. Amesema Mwl.Mwanasala.

Aidha amesema kuwa mafunzo  hayo yataweza kusaidia kuboresha bidhaa za wajasiliamali kwa kuongeza thamani ya bidhaa na ziweze kukubalika  kwenye masoko ya ndani na ya nje.

Post a Comment

Previous Post Next Post