SERIKALI YA TANZANIA NA BRAZIL KUSHIRIKIANA KUENDELEZA SOKA NCHINI PAMOJA NA CHUO CHA MICHEZO MALYA

  

………………………………………………………..

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa   amesema Nchi ya Brazil ipo tayari kushirikianana kitaalamu na  Tanzania katika kukuza Mchezo wa Soka Nchini pamoja na Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya iliyopo Jijini Mwanza kwakufanya Programu ya kubadilishana Wakufunzi wa michezo.

 Mhe Bashungwa amesema hayo Mei 21, 2021Jijini Dar es Salaam  alipokutana na Balozi wa nchi hiyo Mhe. Antonio Augusto Martins Cesar ambapo  amemuomba Mhe. Balozi huyo  kuialika timu ya Taifa ya  Wanawake ya nchi hiyo  kuja kucheza na Timu ya Taifa ya Wanawake ya hapa nchini ili kuleta Motisha ya kukuza Michezo ya wanawake ikiwa ni sehemu ya kutimiza Maagizo aliyoyatoa Mhe. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hivi karibuni Bungeni Jijini Dodoma.

Naye  Balozi huyo  amemshukuru Waziri  Mhe. Bashungwa kwa kupata muda wa kuonana nae ambapo  amepokea maombi ya ushirikiano baina ya Brazil na Tanzania Katika sekta ya Michezo na Kuahidi kuwasiliana na Serikali yake mapema iwezekanavyo ili kujua ni jinsi gani wanaweza kufanya mabadilishano ya wakufunzi wa michezo na pia kukaa na Idara ya Michezo kuainisha ni namna gani wanaweza kukisaidia Chuo cha Maendeleo ya Michezo Nchini.

Aidha , Balozi huyo ameridhia  kuialika timu ya Taifa ya Wanawake ya nakuahidi kulifayia kazi suala hilo

Post a Comment

Previous Post Next Post