Sanamu ya faru fausta kukamilika Septemba

 


Naibu Kamishna wa Uhifadhi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), Dk. Christopher Timbuka, amesema ameridhishwa na hatua iliyofikiwa ya utengenezaji wa sanamu ya Faru Fausta aliyefariki Desemba 2019 akiwa na miaka 56.

Dk. Timbuka amesema hayo baada ya kutembelea chuo cha Lorenzo Academy kilichopo makumbusho ya viumbe hai jijini Arusha akiwa ameambatana na baadhi ya wajumbe wa Menejimenti ya NCAA.

“Tumeridhishwa na hatua iliyofikiwa ya utengenezaji wa sanamu ya Faru Fausta aliyefariki mwaka 2019 akiwa na miaka 56 ambapo alikuwa faru aliyeishi miaka mingi kuliko faru wote Duniani.” Dk. Timbuka

Kwa Mujibu wa wataalamu wa chuo hicho wamesema utengenezaji wa sanamu ya Faru huyo unatarajiwa kukamilika mwezi Septemba mwaka huu ambapo NCAA wataichukua na kwenda kuhifadhi katika makumbusho ya Olduvai Gorge ili kutunza historia yake.

  

Post a Comment

Previous Post Next Post