PUMA ENERGY YATOA ELIMU YA USALAMA BARABARANI KWA WATUMIAJI WA VYOMBO VYA MOTO

 

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mafuta ya Puma Tanzania Dominic Dhanah akizungumza na waandishi wa habari kuhusu watumiaji wa vyombo vya moto barabarani.kuheshimu sheria za usalama barabarani sambamba na kuhamasisha spidi 30 maeneo ya mkusanyiko wa watu

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mafuta ya Puma Tanzania Dominic Dhanah akiwahudumia  watumiaji wa vyombo vya moto barabarani kwa kutoa elimu kuhusu kuheshimu sheria za usalama barabarani sambamba na kuhamasisha spidi 30 maeneo ya mkusanyiko wa watu   

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mafuta ya Puma Tanzania Dominic Dhanah akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi mabalozi wa usalama barabarani waliokuwa wakitoa elimu  kuhusu watumiaji wa vyombo vya moto barabarani.kuheshimu sheria za usalama barabarani sambamba na kuhamasisha spidi 30 maeneo ya mkusanyiko wa watu

Neema Swai( aliyevaa kofia wanne kutoka kulia) wa Shirika la Amend ambalo limejikita kutoa elimu ya usalama barabarani akiwa na wanafunzi ambao ni.mabalozi wa usalama wakitoa elimu kwa wateja wa liofika kujaza mafuta Kituo cha Puma Energy Tanzania

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mafuta ya Puma Tanzania Dominic Dhanah akionesha moja ya chaoisho la alama za barabarani  kuhusu watumiaji wa vyombo vya moto barabarani.kuheshimu sheria za usalama barabarani sambamba na kuhamasisha spidi 30 maeneo ya mkusanyiko wa watu

Picha zikionesha matukio mbalimbali yaliyojiri katika zoezi hilo la kutoa elimu ya usalama barabarani kwa watumiaji wa vyombo vya moto.

  

Sajenti Faustina Ndunguru kutoka Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani akizungumza kuhusu maadhimisho hayo huku akisisitiza madereva kuzingatia sheria ili kuepuka ajali

 

Na Mwandishi Wetu

KAMPUNI ya Mafuta ya Puma Tanzania imeungana na Umoja wa Mataifa pamoja na Shirika la Afya Duniani kuadhimisha Maadhimisho ya Wiki Usalama Duniani, ambapo imetoa rai kwa wanaotumia vyombo vya moto barabarani kuzingatia sheria ili kuepuka ajali.

Kwa mujibu wa Puma Tanzania ni kwamba miongoni mwa operesheni zinazosisitizwa kwa sasa ni kuzingatia mwendo wa ‘sipidi’ 30 katika maeneo mahususi yenye mikusanyiko ya watu wengi yakiwemo ya ibada, sokoni na maeneo ya shule.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mafuta ya Puma Tanzania Dominic Dhanah amesema maadhimisho ya wiki ya usalama yamebebwa na kauli mbiu inayosema ‘Love 30’ikiwa na maana ya kuhamasisha matumizi ya spidi 30 katika maeneo hayo.

“Barabara ni kichocheo muhimu kwa maendeleo ya kiuchumiu. Mwito wetu Puma Energy Tanzania kwa watumiaji wa barabara hususan madereva wa magari na wapanda pikipiki, ni kuhakikisha wanazingatia sheria za usalama barabarani na kwa muktadha wa kaulimbiu ya Love 30, kila mmoja aheshimu maeneo ya vivuko vya watembea kwa miguu,” amesema.

Ameongeza kampuni yake itaendelea kuwa mdau muhimu katika mapambano dhidi ya ajali za barabarani ili kunusuru maisha ya wananchi hususan wenye mahitaji maalumu wakiwemo wanafunzi.

Kwa upande wake Sajenti Faustina Ndunguru kutoka Jeshi la Polisi Kitengo cha Usalama Barabarani Makao Makuu, amesema kwamba kuheshimu sheria za usalkama barabarani ni hatua muhimu ya kuepusha ajali.

“Katika hili nasi tunaungana na jumuiya ya kimataifa katika kaulimbiu ya ‘love 30’ kwa kuwa ni moja ya njia muhimu za kuepusha ajali.
Amesema endapo dereva au mwendesha pikipiki ataendesha kwa spidi ya 30, ni rahisi kuchukua hatua hata kufunga breki kwa haraka katika maeneo ya vivuko vya watembea kwa miguu.

Ameongeza kinyume chake, endapo dereva atapita akiwa na mwendo zaidi ya 30, ni vigumu kukabilana na ajali au changamoto yoyote ya dharura barabarani.

Kwa upande wa wadau wa usalama barabarani akiwemo Meneja wa Shirika la Amend ambalo limekuwa likishirikiana bega kwa bega na wadau wengine wanaojitoa katika mapambano dhidi ya ajali za barabarani Simon Kalolo, amesema ni muhimu kwa watumiaji wa barabara hususan madereva, kuzingatia kaulimbiu ya ‘love 30’ kwa ajili ya kuokoa maisha watumiaji wengine wa barabara.

Kalolo amesema endapo kila mmoja atazingatia na kutekeleza sheria za usalama barabara, ajali za barabarani zitaendelkea kupungua na uchumi wan chi kupaa kwa maendeleo.

Mwanafunzi Moses Amon anayesoma darasa la sita katika Shule ya Msingi Bunge, Dar es Salaam, ambaye pia ni Balozi wa Usalama Barabarani wa Puma Energy Tanzania, aliwakumbusha madereva kutoa nafasi kwa wanafunzi pindi wanapowakuta wakisubiri kufanya hivyo kwenye vivuko vya waenda kwa miguu barabarani.

“Wanafunzi tumekuwa tukikumbana na changamoto ya ajali mara kwa mara ambazo wakati mwingine zinaweza kuepukika. Tunaomba madereva wawe sehemu ya kuepusha vifo na ulemavu kwetu wanafunzi,” alisema.

Wakati huo huo dereva Muthir Msellem Sheikha, ameziomba mamlaka husika kuongeza alama za barabarani pale ambapo kuna ulazima wa kufanya hio, hususan kuwasaidia wenye mahitaji maalumu.

“Wakati mwingine katika maeneo ya kuvuka watembea kwa migguu, dereva uliye mbele unasimama ili kumpisha mwenye ulemavu au mwanafunzi aweze kupita, lakini dereva aliye nyuma hawezi kumwona kutokana na kimo chake na anaweza kuambua kuendelea na safari na madhara yake ni kumgonga mtembea kwa miguu.

“Katika mazingira kama haya nashauri kuwekwe ama taa au alama maalumu za kumwonyesha dereva aliyoko mbali na eneo analovukia mtembea kwa miguu amwone na kumpa nafasi,” amesema

Post a Comment

Previous Post Next Post