WAFANYAKAZI WA BENKI YA I&M WAMETOA MSAADA WA VITU MBALIMBALI KATIKA KITUO CHA WATOTO YATIMA – KIGAMBONI, DAR ES SALAAM.

 

Bi.Anitha Pallangyo, Meneja Masoko Benki ya I&M wapili kushoto akikabidhi baadhi ya zawadi walizopeleka kwenye kituo hicho cha watoto yatima
Timu ya Benki ya I&M leo walipotembelea kituo cha yatima chini ya mpango wao wa kujitolea wa 'IM for You' kushoto ni Bi. Hellen Mbwana, afisa wa benki kitengo cha ukaguzi, Anitha Pallangyo, meneja masoko, Mlekwa Augustine, huduma kwa wateja, Theresia Nguma kitengo cha malipo, fedha na biashara, na Debora mwakyoma afisa masoko na mawasiliano ya benki.

Timu ya wafanyakazi wa I&M walipotembelea kituo cha watoto yatima cha Lady Fatema kilichopo Mjimwema mageti saba, kigamboni Jijini Dar es salaam.


    Wafanyakazi wa benki ya I&M wakiwa na baadhi ya watoto wa kituo hicho
                        ...................................
DAR ES SALAAM. Wafanyakazi wa Benki ya I&M Tanzania siku ya Jumanne tarehe 11, Mei, 2021, wamejitolea msaada wa vitu mbalimbali kama vile Vyakula, Nguo, Sabuni pamoja na vifaa vya Shule katika moja ya Kituo cha kulea watoto yatima kiitwacho ‘Lady Fatema’  kilichopo Mjimwema mageti saba, Kigamboni Jijini Dar es salaam chini ya mpango wao wa ‘IM FOR YOU’ katika jitihada za kurudisha kwa jamii kupitia mpango huo ambapo wafanyakazi hujitolea kwa jamii kwa njia mbalimbali kama vile kutoa elimu ya fedha na ujasiriamali kwa wanawake na vijana ili waweze kujiajiri pamoja na kusaidia vitu mbalimbali kwa wahitaji.

Wasimaizi wa kituo hicho Bi. Mariam Ramadhan na mmewe Bw. Kalekela Omari Mahmood walianzisha kituo hicho mnamo mwaka 2011 wakiwa na lengo la kusaidia watoto yatima wanaoishi katika mazingira hatarishi wakiwapatia elimu, chakula na hifadhi ya kulala. Mbali na misaada mbalimbali inayopelekwa na wafadhili, kituo hicho kina changamoto ya eneo la kutosha la kuweza kuhifadhi watoto wengi na wa jinsia tofauti kwani kwa sasa imewalazimu kubaki na jinsia ya kiume tu kutokana na ukosefu wa vyumba vya kutosha kwaajili ya watoto hao.

Katika kuadhimisha mwezi mtukufu wa Ramadhani na ikiwa ni wiki ya kuelekea sikukuu ya Eid Al-Fitr, wafanyakazi wa Benki ya I&M waliamua kujitolea vitu hivyo katika kituo cha kulea watoto yatima Mjimwema Kigamboni ili na wao waweze kusheherekea na kufurahia sikukuu ya EID inayotarajiwa kuadhimishwa mwishoni mwa wiki hii kutegemeana na kuandama kwa mwezi. Vilevile wafanyakazi wa Benki ya I&M waliweza kuwapa elimu ya usimamizi wa fedha na ujasiriamali Vijana na Wanawake waliokuwa katika kituo hicho ili iweze kuwasaidia katika usimamizi wa fedha za kituo hicho pamoja na kujiajiri wao wenyewe pindi watakapoanza kijitegemea.

Benki ya I&M kupitia wafanyakazi wake wameweza kufanya kampeni mbalimbali za kusaidia jamii kama vile kujitolea kwa kufundisha wanawake, vijana na wajasiriamali katika kikundi cha Wanawake wajasiriami kilichopo Yombo vituka, Temeke jijini Dar es salaam, vilevile wiki iliyopita wafanyakazi wa Benki hiyo walijitolea damu  ili kusaidia wagonjwa wenye uhitaji wa damu katika Hospitali ya Taifa ya Muimbili.

Post a Comment

Previous Post Next Post