SEKTA YA VIWANDA YAONGOZA KATIKA KUSAJILI MIRADI TIC

 

*Imesajili jumla ya miradi 94 (62.25%)

* Mitaji yake ni zaidi ya dola za kimarekani milioni 46

KATIKA kipindi cha mwezi Julai 2020 hadi Machi 2021, Jumla ya miradi 151 imesajiliwa ambayo inatarajiwa kuwekeza mtaji wa Dola za Marekani milioni 987.04 na kutoa ajira 13,857.

Ameyasema hayo leo Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Dkt.Maduhu Kazi wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za kituo hicho Jijini Dar es Salaam amesema ikilinganishwa na kipindi kama hiki mwaka jana ambapo kituo kilisajili miradi 169, idadi ya miradi imepungua kunatokana na athari za janga la ugonjwa wa korona Duniani.

"Sekta ya viwanda imeendelea kuongoza katika miradi iliyosajiliwa katika kituo cha Uwekezaji Tanzania ambapo imesajili jumla ya miradi 94 (62.25%) yenye mtaji wa jumla ya Dola za Marekani milioni 463.17 (46.9%), na inakadiriwa kutoa ajira kwa watanzania wapatao 9,220". Amesema Dkt.Kazi.

Aidha Dkt.Kazi amesema Katika kipindi cha mwezi Januari hadi Machi, 2021 kituo cha Uwekezaji kimefanikiwa kusajili jumla ya miradi mipya 51 ambapo mtaji unaotarajiwa kuwekezwa wa Dola za Marekani milioni 451 umeongezeka kwa asilimia 63 na ajira mpya 4,272 zinazotarajiwa kuzalishwa zimeongezeka kwa asilimia 3.5 kulinganisha na kipindi kama hicho mwaka jana ambapo kituo kilisajili miradi 54.

Pamoja na hayo Dkt.Kazi amesema katika siku za hivi karibuni wawekezaji wengi na mabalozi na wawekilishi wa mashirika ya kimataifa wameonyesha kufurahishwa na mwenendo wa serikali katika suala zima la kuboresha mazingira ya uwekezaji na tayari wameanza kuonyesha nia ya kusaidia programu mbalombali za maboresho ya mazingira ya uwekezaji nchini.

Post a Comment

Previous Post Next Post