WAZIRI AWESO AWATAKA WATAALAMU WOTE NCHINI KUTUMIA TAALUMA ZAO KWA WELEDI

 

WAZIRI wa Maji, Mhe.Jumaa Aweso,akizungumza wakati akifungua kikao kazi cha siku mbili cha Majadiliano ya Wataalamu wa Sekta ya Maji kati ya Tanzania bara na Zanzibar pamoja na  Wizara ya Maji Nishati na Madini wenye lengo la kubadilishana uzoefu unaofanyika jijini Dodoma.

 

Baadhi ya washiriki wakifatilia hotuba ya WAZIRI wa Maji, Mhe.Jumaa Aweso, wakati akifungua kikao kazi cha siku mbili cha Majadiliano ya Wataalamu wa Sekta ya Maji kati ya Tanzania bara na Zanzibar pamoja na  Wizara ya Maji Nishati na Madini wenye lengo la kubadilishana uzoefu unaofanyika jijini Dodoma.

…………………………………………………………………………………..

Na.Alex Sonna,Dodoma

WAZIRI wa Maji, Mhe.Jumaa Aweso imetoa wito kwa viongozi pamoja na wataalamu wote Nchini, kutumia taaluma zao na weledi ili kulisaidia taifa katika kutekeleza miradi yote inayokusudiwa ili kufikia lengo.

Hayo ameyasema leo April 29,2021  wakati wa akifungua kikao kazi cha siku mbili cha  majadiliano ya wataalamu wa Sekta ya Maji kati ya Tanzania bara na Zanzibar pamoja na  Wizara ya Maji Nishati na Madini wenye lengo la kubadilishana uzoefu.

Mhe.Aweso amewataka wataalamu wa wizara hizo kutoka pande zote mbili kuwa wazalendo na kukubali kutumia elimu yao kwa maslahi ya Taifa na siyo kugeuka kuwa majambazi wa kalamu.

” Niwatake Makatibu Wakuu wa pande zote mbili kutengeneza mfumo utakaoweza kuratibu na kufuatilia kwa karibu miradi yote ya maji inayotekelezwa, wahandisi wakamilishe mirardi kwa umakini na siyo kuleta janjajanja.

Miradi mingi ya Maji haikabidhiwi kwa watalaamu, mfano Zahanati ikikamilika inakabidhiwa kwa madaktari au Shule kwa walimu, ni vema miradi ya maji ikabidhiwe kwa watalaamu siyo kwenye zile Jumuiya za Maji ambazo zimekua zikileta migogoro na kushindwa kutunza miradi yetu,” Amesema Aweso.

Waziri Aweso pia ametoa wito kwa watalaamu wa wizara hizo mbili kutengeneza mpango kabambe wa kulinda vyanzo vya maji lakini pia kutengeneza vyanzo vingi vya maji kwa mustakabali wa Nchi yetu.

Hata hivyo Aweso amepiga marufuku tabia ya mamlaka za maji nchini kubambikizia bili za maji Wananchi akisema jambo hilo ni kinyume na sheria na lina lengo la kuigombanisha serikali na wananchi wao.

“Siku za mwisho wa wiki na zile za sikukuu ofisi zote zimefungwa je, mnataka huyu mwananchi akalipie wapi?, toeni elimu sio tu kumkatia mtu maji na hata mtu akishalipa baada ya kukatiwa maji ana muda maalum wa kurejeshewa ndani ya saa 24, unakuta mtu kalipa lakini kurejeshewa inakuwa kama hisani,”amesema Aweso

 Aweso ameongeza kuwa wananchi wote wanatakiwa kuwa na mwamko katika masuala ya kulipia bili zao za maji kwa wakati na hapa anaeleza zaidi

Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Maji Nishati na Madini Zanzibar, Mngeneza Mzee,amemshukuru Waziri Aweso kwa kukubali kuwafungulia mkutano huo huku akimuahidi kushirikiana na Katibu Mkuu Maji Tanzania bara katika kupeana uzoefu wa kuwatumikia watanzania

Post a Comment

Previous Post Next Post