MKURUGENZI MKUU WA BODI YA UTALII TANZANIA (TTB) ASIMAMISHWA KAZI

 Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dkt. Damas D. Ndumbaro (Mb), amemsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Bi. Devotha Mdachi ili kupisha uchunguzi wa madai ya   ubadhirifu wa fedha pamoja na masuala ya kiutawala yanayohusu Rasilimali Watu katika ofisi yake.


Kufuatia hatua hiyo Mhe. Waziri amemteua Betrita James Lyimo, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi kutoka Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi hiyo hadi pale uchunguzi utakapokamilika.

Aidha, Dkt. Damas Ndumbaro ameielekeza Bodi ya Wakurugenzi ya TTB kuwasimamisha kazi watumishi wengine wanaohusika na tuhuma hizo kwa kuwa suala hilo lipo chini ya  Mamlaka yao ili waweza kupisha uchunguzi dhidi ya madai yanayowakabili.

Hata hivyo, Waziri Dkt. Ndumbaro amesema maamuzi hayo hayahusiani na Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG). Uteuzi huo unaanza rasmi leo tarehe 10 Aprili, 2021.

Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Bi. Devotha Mdachi

Post a Comment

Previous Post Next Post