MAMLAKA YA HIFADHI NGORONGORO NCAA,YAAHIDI KUBORESHA MIUNDOMBINU KATIKA HIFADHI ZAKE

 

……………………………………………………………………………………..
Na Woinde Shizza , ARUSHA
Mamlaka ya Hifadhi Ngorongoro NCAA,imeahidi kuboresha miundo mbinu katika hifadhi zake ili kurahisisha shughuli za utalii na kuwa rafiki kwa wadau wa utalii wanaosafirisha watalii kutembelea hifadhi hizo.
Akiongea wakati akijibu matatizo yaliyoibuliwa na wadau wa utalii katika mkutano wa pamoja uliofanyika jijini Arusha kamishna msaidizi Mwandamizi wa huduma za utalii, Paulo Sifoo alisema suala la ubovu wa barabara katika hifadhi zake linashughulikiwa kwa haraka ili barabara zote korofi ziweze kupitika kwa urahisi katika kipindi chote Cha mwaka mzima .
“Tunaendelea kupambana kupitia mpango kazi wetu ili barabara zote zilizopo hifadhini ziweze kupitika katika msimu wote wa  mwaka, nilengo letu kuhakikisha barabara zetu zinatengenezwa kwa tabaka gumu ili  tatizo  liweze kuisha”alisema
Akiongelea suala la matatizo mengine likiwemo suala la uhaba wa maji hifadhini alisema suala hilo lipo katika mpangokazi wa NCAA kwa kuanza kuvuna  maji ya mvua baada ya jitihada za kuchimba visima kushindikana kutoa maji.
Katika hatua nyingine Sifoo ameonya suala la madereva wa utalii wakiwemo wa NCAA wanaokiuka taratibu za kuendesha gari hifadhini ikiwemo mwendo Kasi ,watachukuliwa hatua stahiki ikiwemo kutozwa faini Kwa mujibu wa sheria za uhifadhi.
Awali Baadhi ya wadau hao wa utalii,Msangi Halifa na Ridas Laizer walisema kuwa tatizo kubwa katika hifadhi ya Ngorongoro ni suala la miundo mbinu ya barabara.
Aidha wadau hao wameishukuru mamlaka hiyo ya Ngorongoro kwa hatua ya kuzifanyia kazi Kero mbalimbali zinazolalamikiwa na wadau wa utakii ambazo zimekuwa zikikwamisha shughuli za utalii katika hifadhi ya Ngorongoro na Olduvai

Post a Comment

Previous Post Next Post