KATIBU MKUU NA NAIBU KATIBU MKUU WIZARA YA NISHATI WAANZA KAZI RASMI

 

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Leonard Masanja akisaini kitabu mara baada ya kuwasili katika Ofisi za Wizara ya Nishati Mtumba jijini Dodoma.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Leonard Masanja na Naibu Katibu Mkuu, Kheri Abdul Mahimbali wakiwa katika mazungumzo mara baada ya kuwasili katika Ofisi za Wizara ya Nishati, Mtumba jijini Dodoma.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Leonard Masanja akizungumza na Menejimenti na baadhi ya watumishi wa Wizara mara baada ya kuwasili katika Ofisi za Wizara ya Nishati, Mtumba jijini Dodoma. Kushoto kwake ni  Naibu Katibu Mkuu, Kheri Abdul Mahimbali na wa kwanza kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Daniel Machunda.

Kamishna wa Petroli na Gesi, Adam Zuberi akizungumza wakati Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Leonard Masanja na Naibu Katibu Mkuu, Kheri Abdul Mahimbali walipofanya kikao na Menejimenti na baadhi ya watumishi wa Wizara mara baada ya kuwasili katika Ofisi za Wizara ya Nishati, Mtumba jijini Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati, Kheri Abdul Mahimbali akizungumza na Menejimenti na baadhi ya watumishi wa Wizara mara baada ya kuwasili katika Ofisi za Wizara ya Nishati, Mtumba jijini Dodoma. Kushoto kwake ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Leonard Masanja na kulia kwake ni  ni Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Daniel Machunda.

Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Daniel Machunda akizungumza wakati Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Leonard na  Naibu Katibu Mkuu, Kheri Abdul Mahimbali walipowasili katika Ofisi za Wizara ya Nishati, Mtumba jijini Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati, Kheri Abdul Mahimbali  akisaini kitabu mara baada ya kuwasili katika Ofisi za Wizara ya Nishati Mtumba jijini Dodoma. Kulia ni  Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Leonard.

……………………………………………………………………..

ü  Wasisitiza Uadilifu, Bidii  na Uaminifu

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Leonard Masanja na Naibu Katibu Mkuu, Kheri Abdul Mahimbali, leo tarehe 8 April, 2021, wameanza kazi rasmi katika Wizara ya Nishati baada ya kuapishwa na  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, kushika nyadhifa hizo  April 6, 2021.

Baada ya kuwasili katika Ofisi za Wizara ya Nishati, viongozi hao walifanya mazungumzo na Menejimenti ya Wizara pamoja na  watumishi.

Akizungumza na Menejimenti ya Wizara pamoja na Watumishi, Katibu Mkuu  Wizara ya Nishati, Mhandisi Leonard Masanja amewataka kufanya kazi kwa  bidii, uaminifu na uadilifu.

Aidha, amewataka watumishi hao kufanya kazi kwa ushirikiano ili Wizara iweze kufanikisha shughuli zake zote, na malengo yaliyopangwa yaweze kutekelezeka kwa urahisi.

Vilevile, amewataka Wakuu wa Idara na Vitengo, kuwa wabunifu ili kuongeza ufanisi katika majukumu yao, na pia kuwawezesha watumishi waliopo chini yao ili wafanye majukumu yao kwa ufanisi.

Pia amewataka Wakuu hao wa Idara na Vitengo, kuweka usawa katika mgawanyo wa majukumu ili kila mtumishi aweze kuwatumikia watanzania kwa nafasi aliyonayo.

Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu, wa Wizara ya Nishati, Kheri Abdul Mahimbali, amewataka watumishi wa Wizara kufanya kazi kwa ushirikiano na kuahidi kutumia uzoefu wake katika sekta ya Nishati ili kufanikisha majukumu ya Wizara.

Post a Comment

Previous Post Next Post