DK KALEMANI AMUAGIZA KATIBU MKUU NISHATI KUKAGUA MATENKI YA MAFUTA DAR ES SALAAM KAMA YANA VINASABA

 






 Charles James, Michuzi TV

WAZIRI wa Nishati, Medard Kalemani ametoa siku mbili kwa Katibu Mkuu Wizara hiyo na Mamlaka ya Udhibiti Nishati na Maji (EWURA) kufuatilia matanki yote ya mafuta mkoani Dar es Salaam kujua kama ya vinasaba na siyo kwamba yamechakachuliwa.

Agizo hilo amelitoa leo jijini Dodoma wakati alipofanya ziara ya kushtukiza kwenye vituo vinavyouza mafuta kukagua kama mafuta wanayouza yana vinasaba au hayana kama ambavyo uvumi wa kutokua na vinasaba ulivyosambaa mtaani.

Dk Kalemani amesema hataki kusikia popote nchini kuwa mafuta yanauzwa bila kuwa na vinasaba na muuzaji yoyote ambaye atakiuka maagizo hayo atachukuliwa hatua kali za kisheria.

" Nitoe maagizo kwako Katibu Mkuu na EWURA kuhakikisha mnafuatilia matanki yote yenye mafuta Dar es Salaam kuangalia kama yana vinasaba ama yamechakachuliwa, hatuwezi kuruhusu mafuta ambayo hayana vigezo na ubora yanauzwa ndani ya Nchi yetu.

Kwa wauzaji wote niwaase msikubali kuchukua mafuta yasiyo na vinasaba ambavyo ndivyo hasa vinavyothibitisha ubora wa mafuta mliyonayo, kama mafuta hayana vinasaba msiagize kuja kuwauzia watu, na tukiona mafuta hayana vinasaba hatua tutaichukulia TBS," Amesema Dk Kalemani.

Post a Comment

Previous Post Next Post