WIZARA YA MALIASILI NA UTALII YAKUTANA NA WANANCHI WA KATA YA MAKUYUNI,WILAYANI MONDULI KUTATUA KERO YA TEMBO KUVAMIA MAKAZI YAO

 

Kaimu Mkurugenzi wa Wanyamapori, Wizara ya Maliasili na Utalii, Pellage Kauzeni akizungumza na wananchi wa kata ya Makuyuni kuhusu jitihada za Serikali za kukabiliana na tatizo la wanyamapori kuvamia makazi ya watu nchini, katika kikao kilichofanyika kata ya Makuyuni, Wilayani Monduli leo.

Diwani wa Kata ya Makuyuni, Elias Odupoi akiwatambulisha Watendaji kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii na Taasisi zake (hawapo pichani) katika kikao na wananchi cha kutatua tatizo la tembo kuvamia makazi ya watu kwenye kata yake kilichofanyika leo.

Wananchi wa Kata ya Makuyuni wakimsikiliza Kaimu Mkurugenzi wa Wanyamapori, Wizara ya Maliasili na Utalii, Pellage Kauzeni (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao kuhusu  jitihada za Serikali za kukabiliana na tatizo la wanyamapori kuvamia makazi ya watu nchini, katika kikao kilichofanyika kata ya Makuyuni, Wilayani Monduli leo.

Mkazi wa Kata ya Makuyuni, Kakesyo Lucas akielezea tatizo la tembo kuvamia makazi yao katika kikao cha wananchi na watendaji wa Wizara ya Maliasili na Utalii kilichofanyika kata ya Makuyuni, Wilayani Monduli leo.

Mkazi wa Kata ya Makuyuni, Thobias Laiza (kushoto) akimuonyesha Kaimu Mkurugenzi wa Wanyamapori, Wizara ya Maliasili na Utalii, Pellage Kauzeni (kulia) picha ya vipimo  vya Xray vya mtoto wake aliyejeruhiwa na tembo katika kikao cha wananchi na watendaji wa Wizara ya Maliasili na Utalii kilichofanyika kata ya Makuyuni, Wilayani Monduli leo.

Kaimu Mkurugenzi wa Wanyamapori, Wizara ya Maliasili na Utalii, Pellage Kauzeni (kushoto) akiteta jambo na Mwandishi wa ITV/RADIO ONE, Asiraji Mvungi mara baada ya kikao cha wananchi na watendaji wa Wizara ya Maliasili na Utalii kilichofanyika kata ya Makuyuni, Wilayani Monduli leo.

Post a Comment

Previous Post Next Post