WIZARA YA KILIMO YAWEKA MKAKATI KUONGEZA USHINDANI SOKO LA DUNIA.

 


.Waziri wa Kilimo Prof. adolf Mkenda akizindua mfumo wa kilimo ujulikanao “Kizimba Business Model ” unalenga kuwaunganisha vijana kufanya kilimo biashara chini ya taasisi ya SUGECO leo mjini Morogoro.Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa SUGECO Bw.Revocatus Kimario.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Sokoine Prof. Raphael Chibunda akizungumza kwenye uzinduzi wa Kizimba Business Model leo Morogoro amesema mfumo huo chini ya SUGECO unalenga kusukuma na kubadili kilimo kuwa cha kibiashara na kuvutia vijana wengi zaidi kushiriki.
Waziri wa Kilimo Prof. Adolf Mkenda (kushoto) akisalimiana na Makamu  Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine Prof. Raphael Chibunda (kulia) leo wakati alipozindua mfumo wa Kizimba Business Model unaolenga kuwaunganisha vijana kufanya kilimo biashara chini ya taasisi ya SUGECO.

Waziri wa Kilimo Prof.Adolf Mkenda akitazama bidhaa inayotengezwa na mjasiliamali Fatma Mbaga (kushoto) chini ya usimamizi wa SUGECO ikiwa ni mkakati wa kukuza biashara ya kuongeza thamani ya mazao ya kilimo.Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji SUGECO Revocatus Kimario.

 

Na Farida Saidy, Morogoro.

Waziri wa Kilimo Prof. Adolf Mkenda amesema Serikali kupitia Wizara ya Kilimo itaendelea kushirikiana na wadau wa kilimo ili kuhakikisha kunakuwa na mageuzi mapya katika sekta ya Kilimo kwa kufanya utafiti wa mbegu bora za Kilimo ili kuleta tija katika Kilimo kwa ajili ya kuongeza ushindani katika soko la dunia

Waziri wa Wilimo Prof Mkenda alisema hayo katika ziara yake mkoani morogoro wakati wa kuzindua mkakati mpya wa kilimo  kwa utaratibu wa kizimba ulioandaliwa na sokoine university graduate entrepreneurs cooperative [SUGECO] tukio ambalo limewashirikisha wadau mbalimbali wenye nia ya kuleta mageuzi kwenye kilimo

Alisema kuwa kilimo kinachangia chini ya theluthi moja ya pato la Taifa licha ya wakulima kukumbana na changamoto kwenye kilimo hivyo wakulima wanahitaji fedha kwa ajili ya kuinua hali zao za maisha katika kuleta mageuzi ya kilimo

Alisema kuwa suala la kuongeza tija katika kilimo litasaidia kuongeza pato la wakulima na Taifa kwa ujumla, kuna haja ya kuongeza tija kwenye kilimo ili kuwa na ushindani duniani pamoja na kusimamamia mauzo ya mazao ili kuongeza faida kwa wakulima

“Bila mbegu nzuri huwezi kuzalisha vizuri, tunahitaji matumizi bora ya pembejeo na teknolojia ikiwa ni pamoja na umwagiliaji na namna ya kuwafikia watu tunahitaji mfumo huu wa kizimba tuliozindua leo kuharakisha namna ya kwenda haraka kuwafikia wakulima na kuleta matokeo chanya ambayo itasambaa kwa watu na kuchukua kama mfano” alisema prof mkenda 

Alisema kuwa mkakati wa kizimba ulipaswa kuanza mapema zaidi ili kusonga mbele katika maendeleo ya kilimo, hivyo amesema kuwa vijana wanapaswa kupewa kipaumbele katika uzalishaji wa mazao endapo kama watawezeshwa kupata ardhi pamoja na mitaji

Katika mpango mpya wa kizimba wanapaswa kupeana uzoefu na ushirikiano wa kutosha ili kuzalisha zaidi ambapo wananchi wanahitaji fedha katika kukuza uzalishaji huku akiwaomba wadau wa bank kutoa mikopo kuwezesha wakulima kuzalisha mazao na kutengeneza kwa wakulima wanapozalisha mazao yao na uhakika wa kupata masoko

Alisema kuwa sekta ya kilimo ni miongoni mwa sekta zinazoajiri watu wengi zaidi ni muhimu kupewa kipaumbele kutumika kama nguvu kazi ya taifa huku akieleza changamoto kubwa inayokwamisha vijana ikiwa ni kukosa mitaji pamoja na ardhi kwa ajili ya uzalishaji wa mazao

Aidha prof mkenda alisema kuwa katika maeneo ya vijini hasa katika maeneo yenye changamoto ya hali ya hela na uhaba wa mvua, inaonesha hali halisi ya maisha ya wakulima hivyo utaratibu wa vizimba utasaidia kuongeza tija katika kilimo

Wakati huohuo ametoa wito kwa Halmashauri zote hapa nchini wasaidie namna ya kusogeza kilimo kwa kuwa wakulima wengi wanalima bila kuwa na uhakika wa masoko na kuuza mazao yao hivyo wajenge mazingira ya kutengeza hela ili kupata faida

“Nawapongeza halmashauri ya nzega kutoka hekta 40, kibiti hekta 1000, mvomero hekta 1500,na halmashauri ya liwale wametoa hekta 300 huu ni uthubutu wa pekee sana kuongeza tija kupitia ardhi hii” alisema prof mkenda

Kwa upande wake mwenyekiti wa bodi ya SUGECO Dkt Anna Temu amewapongeza SUGECO  kubuni mbinu ya kukuza kilimo na kuwaomba waishi katika jamii ya wakulima na wafugaji ili kujikita na mbinu za kuondoa umaskini ambayo ndio kipaumbele cha sugeco katika mkakati wao kubuni mpango huo

Nao wanufaika wa SUGECO Bwana Yohana Itayo na Fedrick Jonathan wameiomba serikali kupanua wigo kusaidia vijana ili kupata ujuzi kwa vitendo kushirikiana na wakulima wenye uzoefu hivyo wameshauri vijana wanaomaliza vyuo wapelekwe kupata uzoefu wa kuanzisha mashamba yao wenye

joseph Masimba ni Afisa Meneja uendeshaji wa SUGECO amesema kuwa kizimba ni mfumo wa kuzalisha kwa pamoja ambao unaziweka rasilimali zote kwa pamoja kujumuisha mabank, wadau wa maendeleo kilimo lengo ikiwa ni kushughulikia changamoto zinazoikumba sekta ya kilimo hasa tatizo la tija, vijana kukosa ardhi na mitaji katika uzalishaji mazao ya kilimo

Post a Comment

Previous Post Next Post