Na Zuena Msuya, Simiyu
Waziri wa Nishat, Dkt. Medard Kalemani ameweka jiwe la msingi na kuzindua Ujenzi wa Kituo cha Kupoza Umeme cha Imalilo kilichopo wilayani Bariadi mkoani Simiyu.
Akizungumza wakati wa akiweka jiwe la Msingi, Machi 3, 2021,
Dkt. Kalemani amesema kuwa Ujenzi wa kituo hicho utakamilika ndani ya kipindi cha mwaka mmoja kuanzia sasa.
Aidha alisema kuwa ujenzi wa kituo hicho unatekelezwa na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kwa kutumia fedha za ndani shilingi Bilioni 75.
Vilevile alisema kuwa Serikali imetoa kiasi cha zaidi ya shilingi Milioni 47, kwa ajili ya kuwalipa fidia Wananchi walipisha eneo la mradi huo.
Kituo hicho kitakapokamilika kitakuwa na uwezo wa kizalisha takribani Megawati 100, zitakazo tumika ndani ya mkoa huo na mikoa jirani.
" umeme utakaozalishwa hapa ni mkubwa utauwezesha mkoa huu na mikoa jirani kuendesha shughuli za viwandana, na uwekezaji wa aina yoyote unaohitaji umeme mwingi", alisema Dkt. Kalemani.
Amesema TANESCO wamekuwa wamekuwa wakitekeleza miradi kama hiyo nchi nzima ambapo mpaka sasa tayari wamejenga Vituo vikubwa kama hicho wanatekeleza miradi mingine kama hiyo 24 kati ya 134 vinavyotarajiwa kujengwa nchi nzima.
Dkt.Kalemani aliaguza kuwa, kazi zote zisizohitaji taaluma maalum ikiwemo ya vibarua, wapewe vipaumbele watu wanaozunguka eneo hilo maeneo Jirani kwa kuwa ndiyo walinzi wakubwa wa mradi huo.
Hata hivyo alitoa siku mbili kwa TANESCO, kukamilisha kulipa fidia watu Watano ambao bado hawajalipwa fidia kutokana na changamoto ya majina kutofautia katika vitambulisho, Hundi pamoja na nyaraka za malipo.
Aliwatoa hofu wananchi hao kuwa tayari changamoto hiyo imetatuliwa na muda wote watalipwa fedha zao kwa kuwa zipo tayari.
Kuhusu usambazaji wa Umeme vijijini, aliwaeleza wananchi wa mkoa huo, kujiandaa kwa kutandaza nyaya katika nyumba zao kwa kuwa mradi wa usambazaji wa Umeme Vijiji (REA III) mzunguko wa pili itamaliza usambazaji wa Umeme katika vijiji vyote nchini ambavyo bado havijafikiwa na Umeme.
Aliwasisitiza kuwa bei halisi ya kuunganishiwa Umeme ni shilingi 27,000 tu.
Na zoezi hilo litakamilika ndani ya miezi 24, kusambaza vijiji vyote nchini.
Waziri wa Nishat, Dokta Medard Kalemani akiweka jiwe la msingi na kuzindua Ujenzi wa Kituo cha Kupoza Umeme cha Imalilo kilichopo wilayani Bariadi mkoani Simiyu,Dkt. Kalemani amesema kuwa Ujenzi wa kituo hicho utakamilika ndani ya kipindi cha mwaka mmoja kuanzia sasa.