TBS IMEENDELEA KUTOA ELIMU KUHUSU VIWANGO KATIKA WILAYA YA MUSOMA MKOANI MARA

 Mfanyabiashara wa Duka la Chakula, Mama Mary (kulia) akionesha cheti chake cha usajili wa duka la chakula wakati maafisa wa TBS wakitoa elimu ya usajili wa majengo ya chakula na vipodozi kwa wafanyabiashara waliopo soko kuu na stendi kuu ya mabasi wilayani Musoma.

Afisa udhibiti ubora,Mhandisi Emmanuel Shilinde (TBS),akiwaasa wafanyabiashara Musoma waliopo katika soko la Nyasho mlango mmoja kutokuuza nguo za ndani za mitumba kwani haziruhusiwi ili kuepuka hasara na kuwahimiza waliopo Nyasho soko kuu kusajili majengo ya chakula na vipodozi

Wanafunzi wa shule ya msingi Mwisenge A wilayani Musoma wakipatiwa elimu ya viwango itakayowasaidia kuwa mabolozi wazuri wa masuala ya ubora.

Wanafunzi wa shule ya msingi Mwisenge A wilayani Musoma wakipatiwa elimu ya viwango itakayowasaidia kuwa mabolozi wazuri wa masuala ya ubora.

*******************************

Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limeendelea kutoa elimu ya viwango vya ubora wa bidhaa katika wilaya ya Musoma ambapo imeweza kukutana na Wafanyabiashara mbalimbali pamoja na wanafunzi na kuwahimiza kutumia bidhaa zenye ubora ili kuweza kumlinda mlaji.

Akizungumza mara baada ya kutembelewa na maafisa wa TBS ofisini kwake, Mkurugenzi wa halmashauri ya Manispaa ya Musoma Mjini, Bi.Fidelica Myovella ameipongeza TBS kwa kutoa elimu kwa wananchi katika ngazi ya Wilaya.

“Elimu hii mnayoitoa TBS itaongeza ufahamu na kuhakikisha suala la uuzaji wa bidhaa hafifu sokoni linapungua kama sio kwisha kabisa”. Alisema Bi.Fidelica.

Pamoja na hayo TBS imetoa elimu ya viwango pia kwa wanafunzi na walimu wa shule ya Sekondari ya Ufundi Musoma, Mwisenge pamoja Bweri wilayani humo ambapo muitikio wa uelewa wa elimu hiyo ni kubwa.

Post a Comment

Previous Post Next Post