Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Zainab Telack akifafanua jambo kwa Mkurugenzi wa Shirika la Reli Nchini Bw. Masanja Kadosa wa kwanza kushoto walipofika eneo la viwanda Manispaa ya Shinyanga ili kujionea namna gani reli hiyo inavyoweza kusaidia usafirishaji wa mazao na bidhaa za viwanda huku Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga katikati Bi. Yasinta Mboneko akifuatilia kwa makini.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Zainab Telack akifafanua jambo kwa Mkurugenzi wa Shirika la Reli Nchini Bw. Masanja Kadosa wa kwanza kushoto walipofika eneo la Bandari Kavu ya Isaka ili kujionea namna gani upanuzi wa bandari hiyo utakavyoleta ufanisi wa biashara na ukwezezaji katika mikoa ya kanda ya Ziwa, wengine katika Picha ni Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Bi. Yasinta Mboneko na Katibu Tawala Mkoa Shinyanga Bw. Albert Msovela.
Mkurugenzi wa Shirika la Reli Nchini Bw. Masanja Kadosa wa kwanza kushoto akiongea jambo katika eneo la Bandari Kavu ya Isaka ili kujionea namna gani upanuzi wa bandari hiyo utakavyoleta ufanisi wa biashara na ukwezezaji katika mikoa ya kanda ya Ziwa.
………………………………………………………………………………………………….
Na Anthony Ishengoma
Serikali imeanza ujenzi wa kipande cha Reli ya kisasa ya SGR kwa kipande cha Isaka-Mwanza chenye thamani ya Dora za Kimarekani Bil.1 mradi ambao utakuwa wa na manufaa makubwa kwa Nchi jilani za Uganda, Rwanda na Burundi pamoja na mikoa ya Kanda ya Ziwa.
Akiongea wakati wa kutambulisha ujenzi wa mradi Mkurugenzi wa Shirika la Reli nchini Masanja Kadogosa alitaja faida za mradi huo kwa wakazi wa Kanda ya Ziwa kuwa utarahisisha usafiri kwa wakazi hao kwenda Dodoma na Dar es salaam lakini pia Bandari Kavu ya Isaka itatumika kupokea na kushusha mizigo yote ya Nchi jilani.
Bw. Kadogosa aliongeza kuwa ujenzi wa reli hii ya kisasa utaenda sambamba na upanuzi wa Bandari kavu ya Isaka kwa lengo la kuiongezea ufanisi kwa kuhakikisha Nchi za jirani zitakapoagiza mizigo ziwe zinapokelea mizigo yake Isaka moja kwa moja tofauti na sasa ambapo mizigo inafuatwa Dar es Salaam.
Aidha Bw. Kadogosa alisema pamoja na kuwepo kwa faida hizo lakini pia shughuli za ujenzi wa reli hiyo ni fursa kubwa kwa wakazi wa Shinyanga kwani watapata ajira na ujuzi kwa kushiriki katika mradi huu mkubwa utakaoa chukua miezi 36 mpaka kukamilika kwake.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Zainab Telack akiongea katika bandari kavu ya Isaka alitaka ujenzi wa reli hiyo kuzingatia na kujenga kipande cha reli kuelekea eneo la viwanda lililopo Manispaa ya Kahama na kuongeza kuwa upanuzi wa Bandari Kavu ya Isaka utavutia zaidi wawekezaji ambapo tayari wawekezaji katika saruji na kiwanda cha nguo wako tayari hivyo upanuzi wa bandari hiyo ni muhimu kwa wawekezaji wa mkoa huo.
Aidha Bi. Telack alihaidi kutoa ushirikiano katika nyanja zote zinatakiwa kufanyiwa kazi ikiwemo kuwa andaa wananchi kupokea mradi huo lakini pia kushirikiana na shirika la reli kutatua changamoto zitakazojitokeza ikiwemo suala la ardhi na kuhamisha baadhi ya miundombinu itakayoingiliana na ujenzi huo.
Aidha diwani wa Kata ya Isaka Bw. Pazi Majuto Pazi aliongeza kuwa ujenzi wa Reli mpya na ya Kisasa ni fursa kwa wakazi wa Isaka kujipatia Ajira katika mradi wa ujenzi lakini akawa na wasiwasi na baadhi ya wageni ambao tayari wako Isaka kusaka ajira hiyo kuwa wanaweza kuwakosesha fursa wakazi wa eneo lake la utawala.
Ujenzi wa reli ya kisasa ni mwendelezo wa ujenzi wa reli hiyo hapa Nchini ambao tayari inaendelea kwa kipande cha Dar es Salaam-Morogoro na Morogoro- Makutopola Singida.