GST YAANZA MAJADILIANO NA STAMICO JUU YA KUWASAIDIA WACHIMBAJI WADOGO WA MADINI NCHINI

**********************************

Na.Samwel Mtuwa- Singida

Leo Machi 7, 2021 Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) imeanza majadiliano na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) juu ya Ushirikiano wa namna bora ya kuwasaidia wachimbaji wadogo wa Madini katika Utafutaji , Uchimbaji na Uchenjuaji Madini.

Katika majadiliano hayo yanayofanyikia mkoani Singida GST inawakilishwa na timu ya wataalamu watano waliobobea katika Sekta ya Madini nchini.

Mwanzo wa majadiliano haya kutapelekea kufanyika kwa makubaliano maalum (MoU) baina ya GST na STAMICO ya kuwasaidia wachimbaji wadogo wa Madini ili waweze kufanya shughuli zao za Utafutaji , Uchimbaji na Uchenjuaji madini wenye tija kwa lengo la kuendeleza sekta ya Madini nchini.

Pamoja na majadiliano hayo Machi 8, 2021 GST inatarajia kutoa mrejesho (Feedback) mkoani Singida juu ya Utafiti wa Madini uliofanyika mkoani hapo katika wilaya ya Mkalama.

 

Post a Comment

Previous Post Next Post