BODI YA NISHATI VIJIJINI YATEMBELEA MRADI WA UJENZI KITUO CHA KUPOZA NA KUSAMBAZA UMEME CHA IFAKARA

 

Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Wakili Julius Kalolo wa pili kushoto akiongoza kikao cha majadiliano ya utekelezaji wa Mradi wa ujenzi wa kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Ifakara wakati wa ziara ya Bodi hiyo kukagua Mradi huo iliyofanyika tarehe 05/03/2021. Anayemfuatia kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini, Mhandisi Amos Maganga akifuatiwa na Mkurugenzi wa REB, Mhandisi Styden Rwebangila

Wakurugenzi wa Bodi ya Nishati Vijijini wakipewa maelezo ya ujenzi wa Mradi wa kituo ch kusambaza na kupoza umeme cha Ifakara. Aliyepo kushoto akitoa maelezl ni Mhandisi wa AEE Power, Charlse Macharia na kulia ni Meneja Msimamizi wa Mradi, Jose maroquin

Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Wakili Julius Kalolo (aliyepo katikati) akiongea na wafanyakazi wa Kampuni ya AEE Power inayotekeleza Mradi wa Ujenzi wa kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Ifakara wakati ya ziara ya ukaguzi ya Mradi huo iliyofanyika tarehe 05/03/2021 wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Wakili Julius Kalolo (aliyepo katikati) akiongea na wafanyakazi wa Kampuni ya AEE Power inayotekeleza Mradi wa Ujenzi wa kituo cha kupooza na kusambaza umeme cha Ifakara wakati ya ziara ya ukaguzi ya Mradi huo iliyofanyika tarehe 05/03/2021

…………………………………………………………………………………….

Bodi ya Nishati Vijijini (REB) imefanya ziara ya kukagua utekelezaji wa ujenzi wa Mradi wa kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Ifakara.

Ziara ya Bodi ilifanyika tarehe 05 Machi 2021 katika kituo hicho kilichopo Ifakara Mkoani Morogoro.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Wakili Julius Kalolo amesema Mradi huo ukikamilika utawezesha Wilaya ya Kilombero na Ulanga kupata umeme wa uhakika.
Aidha alisema kuwa upatikanaji wa nishati ya umeme wa uhakika utawezesha kuanzishwa kwa viwanda na kuboresha utoaji wa huduma za afya, elimu, maji na uanzishwaji wa biashara ndogondogo hivyo kuongeza pato la Serikali na ajira.
”Na kwa njia hiyo tutapata umeme pamoja na huduma za kijamii zitapatikana sababu umeme huo utapekekwa katika vituo vya afya, zahanati, mashule ,taasisi za kidini na kwenye viwanda” am
alisema Wakili Kalolo

Wakili Kalolo alisema kuwa nishati hiyo ya umeme itasambazwa katika miradi ya maji hivyo kuongeza upatikanaji wa maji safi na salama vijijini.

Post a Comment

Previous Post Next Post