TBS IMEANDAA MAFUNZO KWA WAZALISHAJI,WAUZAJI NA WASAMBAZAJI WA MABATI NA KOILI ZA MABATI

 

Kaimu Mkurugenzi Mkuu TBS Bw.David Ndibalema akifungua mafunzo yanayohusu viwango na matakwa  ya viwango vya mabati na koili yaliyofanyika leo katika makao makuu ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Jijini Dar es Salaam.

mafunzo yanayohusu viwango na matakwa  ya viwango vya mabati na koili yaliyofanyika leo katika makao makuu ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Jijini Dar es Salaam.

Wazalishaji,wauzaji,wasambazaji wa mabati na wadau mbalimbali wakifuatilia mafunzo yanayohusu viwango na matakwa ya viwango vya mabati na koili yaliyofanyika leo katika makao makuu ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Jijini Dar es Salaam.

*************************************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Shirika la Viwango Tanzania TBS limetoa mafunzo kwa wazalishaji,waagizaji,wasambazaji na wadau mbalimbali wa mabati na koili za mabati hapa nchini baada ya Tanzania kukamilisha utaratibu wa kupitisha viwango vya mabati na koili ambavyo ni TZS 353:2020/EAS 11:2019 na TZS 1477:2020/EAS 468:2019 kuwa viwango vya kitaifa pamoja na kiwango Na.1476:2017.

Akizungumza wakati anafungua mafunzo hayo Kaimu Mkurugenzi Mkuu TBS Bw.David Ndibalema amesema shirika hilo lilifanya tathimini ambapo ilibaini kuwa yapo mabati na koili za mabati zinazozalishwa na kuaingizwa hapa nchini hazikidhi matakwa ya viwango.

“Mafunzo haya yanalenga kuandaa washiriki kuwa wenye mwelekeo mzuri zaidi na wa liuweledi katika kuzalisha,kuingiza na kusambaza mabati na koili za mabati zinazokidhi matakwa ya viwango”. Amesema Bw.Ndibalema.

Aidha Bw.Ndibalema amesema TBS itaendelea kutilia mkazo kusimamia maswala ya viwango na udhibiti ubora na kwamba biashara zinafanywa katika mifumo inayoeleweka na kukubalika kisheria sambamba na kanuni zinazosimamia mifumo viwango na udhibiti ubora.

Post a Comment

Previous Post Next Post