Waziri wa maji Jumaa Aweso akiongea na watumishi wa sekta ya maji wa mkoa wa Arusha.
*************************************
NA NAMNYAK KIVUYO, KIVUYO
Waziri wa maji Jumaa
Aweso amesema wizara ya maji haitakuwa kero kwa wananchi kwani watafanya
kazi usiku na mchana kuhakikisha wanatatua changamoto zote za maji.
Aweso aliyasema hayo
wakati akizungumza na watumishi wa sekta ya maji wa mkoa wa Arusha
ambapo aliesema kuwa kazi ya kushughulikia changamoto za maji
haijawashinda wanaweza kutekeleza na fahari yao itakuwa ni kuona
wananchi wanapata maji.
Alisema kuwa
maendeleo ya sekta ya maji yanaanza na watumishi hivyo wakashirikiane
katika kutatua changamoto za maji huku wakitekeleza majukumu yao kwa
ukamilifu ili kutimiza hadhma ya upatikanaj wa maji safi na salama kwa
wananchi.
Alisema dhamira ya serikali ni kupatikana kwa
huduma muhimu ya maji safi salama ya yakutosheleza wananchi ambapo
serikali imekusudia kutenga bajeti ya utekelezaji wa miradi ya maji
ikiwamo mradi mkubwa wa maji unaoendelea kutekelezwa mkoani Arusha.
“Kazi haijatushinda tutafanya kazi usiku na
mchana kuhakikisha maji yanapatikana maeneo yote yaliyo katika Mpango na
katika hili niwaambie tu kuwa mhandisi yoyote ambaye anayefikiria kuwa
yupo kwaajili ya kukwamisha wizara ya maji ajue kuwa anajikwamisha
mwenyewe,”Alisema Aweso.
Alisema uhuni unaofanywa na baadhi ya watendaji
ili kuhujumu miradi hivyo wakahakikishe wanafanya kazi inavyostahili ili
kutekeleza adhima ya Rais lakini pia ilani ya chama cha mapinduzi (CCM)
kwa kuhakikisha wananchi wote wamapata huduma ya maji.
Kwa upande wake mkuu wa Mkoa wa Arusha Iddi
Kimanta aliwataka watumishi wa secta ya maji kutekeleza wajibu wao
kazini na sio kusubiri kusukumwa kwani maji ni moja ya sekta ambayo
inamgusa mtu moja kwa moja.
Aliwasihi kuisaidia serikali kutekeleza majukumu
yake kwa weledi wa hali ya juu pamoja na kuwashirikisha viongozi wa
serikali changamoto zinazowakabili.
Naye Mkurugenzi wa mamlaka ya maji na usafi wa
mazingira (AUWSA) Mhandisi Justin Rujomba aliahidi kukabidhi mradi wa
maji wa Moita ifikapo April 9 mwaka huu ambapo watatekeleza kwa wakati
na kwa ubora.