NAIBU KATIBU MKUU AONGOZA SEKTA YA MAJI KATIKA MAADHIMISHO YA MEI MOSI NJOMBE

Mwandishi Wetu,

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Rose Ambrose, ameiongoza Sekta ya Maji katika Maadhimisho ya  Siku ya Wafanyakazi Duniani,  Mei Mosi yaliyofanyika kitaifa mkoani Njombe.

Sekta ya Maji, ikijumuisha Wizara pamoja na taasisi zake, imeshiriki maandamano ya Mei Mosi kwa kuonesha huduma na miradi mbalimbali inayotekelezwa  katika kuhakikisha upatikanaji wa huduma ya majisafi na salama kwa wananchi.

Maadhimisho ya Mei Mosi 2026 yakiwa nab kaulimbiu: “Kazi Zenye Staha ni Nguzo Imara kwa Maendeleo Endelevu katika Utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050.” yamehudhuriwa na Mgeni Rasmi, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Katika hafla hiyo, mtumishi Ibrahim David , Afisa  Kumbukumbu amepewa Tuzo ya Mfanyakazi Hodari wa Wizara ya Maji kwa mwaka 2026, kwa kutambua weledi, uadilifu na mchango wake katika utendaji kazi.


Post a Comment

Previous Post Next Post