Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula leo tarehe 21 Februari, 2021 ameongoza mjadala kuhusu fursa na changamoto kwenye uchimbaji na biashara ya madini ya vito katika Mkutano wa Kimataifa wa Uwekezaji katika Sekta ya Madini unaoendelea katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.
Mkutano huo ulioandaliwa na Wizara ya Madini unahusisha wadau wa madini ikiwa ni pamoja na Taasisi za Serikali, Taasisi za Kifedha, kampuni za uchimbaji wa madini, wachimbaji wadogo wa madini, wafanyabiashara wa madini nk.
Kauli mbiu ya Maonesho ni "Sekta ya Madini kwa Uchumi Imara na Maendeleo Endelevu."