Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari (ICT) – Mhe. Mhandisi. Andrea Mathew Kundo pamoja na Maafisa wa wizara hiyo pamoja na maafisa kutoka UCSAF, TCRA-CCC, TCRA, wakizungumza na Wajumbe wa Kamati Tendaji ya Vodacom Tanzania PLC, wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Hisham Hendi (kwenye runinga) wakati wa ziara ya naibu waziri, alipozuru makao makuu ya Vodacom Tanzania jijini Dar es salaam. Lengo la ziara hiyo likiwa ni kufahamiana pamoja na kujadili njia za kuongeza thamani ya mteja na kuhakikisha ufanisi wa utendaji.
Mkurugenzi wa Biashara Vodacom Tanzania PLC, Linda Riwa akizungumza kwenye mkutano uliowakutanisha Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari (ICT) – Mhe.Mhandisi. Andrea Mathew Kundo, Wajumbe wa kamati Tendaji ya kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania PLC na Maafisa kutoka UCSAF, TCRA-CCC na TCRA.
Mkurugenzi wa Kitengo cha Mtandao cha kampuni ya Vodacom Tanzania PLC, Andrew Lupembe akizungumza kwenye mkutano huo kuhusu namna kampuni hiyo inavyoendelea kutanua na kuboresha mtandao wake ili kutoa huduma bora kwa wateja wa kampuni hiyo.