Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petrol Nchini (TPDC) Dkt.James Mataragio akizungumza na waandishi Habari wa wakati wa alipotembelea mradi wa utandikaji mabomba ya gesi asilia Majumbani katika Mtaa wa Sinza Mori jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC Dkt.James Mataragio akipata maelezo kutoka kwa mkandarasi anayetekeleza mradi wa utandikaji wa mabomba ya Gesi asilia Majumbani katika Mtaa wa Nzasa Sinza Mori jijini Dar es Salaam.
Uchimbaji wa mitalo kwa ajili ya kutandika mabomba ya gesi asilia majumbani ukiendelea katika Mtaa wa Nzasa Sinza Mori jijini Dar es Salaam.
*Mkandarasi aahidi kumaliza mradi ndani ya miezi sita badala ya mwaka Mmoja .
Na Chalila Kibuda,Michuzi Tv.
SHIRIKA la Maendeleo la Petroli nchini (TPDC) limesma kuwa baada ya kauli ya Waziri wa Nishati Dkt.Merdad Kalemani kuharakisha mradi wa usambazaji wa gesi majumbani ,Shirika hilo limekutana na mkandarasi wa utandikaji wa mabomba ambapo mradi huo utachukua miezi sita badala ya mwaka mmoja.
Akizungumza wakati wa Ukaguzi mradi wa kutandika mabomba ya gesi Sinza Mori Mtaa wa Nzasa kwa ajili Gesi ya majumbani Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC Dkt.James Mataragio amesema kuwa baada ya kutembelea mradi huo na ahadi ya mkandarasi wanahakikisha mradi huo utakamilika kwa wakati.
Mradi huo utakwenda kutekelezwa Polisi Baracks kurasini ili wananchi wapate huduma ya gesi ambayo ina gharama nafuu.
Amesema kuwa baada ya Serikali kutaka utumiaji bidhaa za ndani lakini kumekuwepo na baadhi ya wazalishaji kuuza kwa bei ya juu sana kuliko kuagiza kutoka nje ya nchi.
Amesema kitendo hicho cha kuuza bei ya juu ni sawa na uhujumu uchumi kwani kutafanya wakandarasi kuagiza nje ya nchi na kufanya nchi kukosa mapato yatokanayo na kodi.
Dkt.Mataragio wamemtaka mkandarasi kwenda kwa haraka kwani wananchi wanasubiri mradi wa gesi majumbani kwa hamu.
Aidha amesema kuwa agizo la Waziri mwenye dhamana ya Nishati wanakikisha mradi unakamilika kwa wakati kutokana walivyojipanga katika kumsimamia mkandarasi wa utandikaji wa mabomba ya gesi majumbani.
Nae Mkandasi BQ Contractors Limited Mhandisi John Bura amesema kuwa mradi huo utakamilika ndani ya miezi sita kutokana na kuwa na uhakika wa mabomba ya kutandika.
Amesema changamoto iliyokuwepo ni kutokana na mabomba hayo kwa ndani kuuzwa bei juu na kusababisha kuagiza nje.
Amesema licha ya kulipa kodi kwa kuagiza nje kuna unafuu mkubwa kuliko kununulia viwanda vya ndani.