TBS YATEKETEZA BIDHAA ZISIZOKIDHI KIWANGO ZENYE THAMANI YA SH.MILIONI 40

 

Mkurugenzi wa udhibiti ubora kutoka shirika la viwango Tanzania TBS Makao Makuu Lazaro Msasalaga akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kumalizika kwa zoezi la kuteketeza bidhaa zisizokidhi kiwango na zilizoisha mda wake katika dampo la kisasa la Chidaya jijini Dodoma.

Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano kutoka Shirika la viwango Tanzania TBS Bi Roida Andusamile akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kumalizika kwa zoezi la kuteketeza bidhaa zisizokidhi kiwango na zilizoisha mda wake katika dampo la kisasa la Chidaya jijini Dodoma.

Mkaguzi kutoka Shirika la viwango Tanzania TBS Domisiano Rutahala akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kumalizika kwa zoezi la kuteketeza bidhaa zisizokidhi kiwango na zilizoisha mda wake katika dampo la kisasa la Chidaya jijini Dodoma.

Bidhaa zisizokidhi kiwango na zilizoisha muda wa matumizi zilizokamatwa na shirika la viwango Tanzania TBS zikishushwa katika dampo la kisasa la Chidaya lililopo jiji Dodoma kwa ajili ya kuteketezwa.

  

Bidhaa zisizokidhi kiwango na zilizoisha mda wake zilizokamatwa na shirika la viwango Tanzania TBS zikiteketezwa leo katika dampo la kisasa la Chidaya jijini Dodoma.

……………………………………………………………………………..

Na Ezekiel Mtonyole – Dodoma.

Shirika la viwango Tanzania TBS kanda ya kati leo limeteketeza bidhaa mbalimbali zilizoisha mda wake na bidhaa ambazo hazijasajiliwa zenye thamani ya shilingi milioni 40 zilizokutwa zikiuzwa katika maduka mbalimbali katika mikoa ya Dodoma, Tabora na Singida.

Akizungumza wakati wa zoezi hilo Mkurugenzi wa udhibiti ubora kutoka TBS Makao Makuu Lazaro Msasalaga amesema bidhaa hizo zilikutwa zikiuzwa katika maduka mbalimbali ambazo ni vipodozi, vyakula na bidhaa nyingi zikiwa ni za watoto jambo ambalo ni hatari kwa kizazi kijacho.

“Tumeteketeza bidhaa hizi ukiangalia bidhaa nyingi ni za watoto sasa hili ni jambo la hatari sana tutajenga kizazi dhaifu sana kitakachokuwa hakina uwezo wa kufanya kazi za kujenga taifa ndio maana tunasisitiza kuzichunguza bidhaa hizo kabla ya kuzitumia” amesema Msasalaga.

Ametoa wito kwa wafanyabiashara nchi nzima kuhakikisha wanajenga utaratibu wa kuzikagua bidhaa zao mara kwa mara ili kubaini bidhaa feki, zilizoisha mda wake na zinazokaribia kumaliza mda wake ili waziondoe katika maduka yao kwani TBS imejipanga kufanya msako nchi nzima kubaini bidhaa hizo.

“Wafanyabiashara tunawataka wajenge utaratibu wa kukagua bidhaa zao mapema ili waziondoe aidha waziuze mapema au kuzitoa au watupe taarifa tuziteketeza bila faini” amesema.

Amesema bidhaa feki zinazoongoza kwa kuuzwa ni vipodozi hivyo amewataka wananchi kujenga utaratibu wa kupitia katika tuvuti ya shirika la viwango Tanzania TBS ili kuona orodha ya vipodozi vilivyosajiliwa kwa matumizi hapa nchini.

Kwa upande wake Mkuu wa kitengo cha mawasiliano Shirika la viwango Tanzania TBS Bi Roida Andusamile amesema TBS  inamajukumu ya kuondoa bidhaa hafifu sokoni na kuziharibu au kuzirudisha zinakotoka pindi zinapobainika kuwa hazifai kwa matumizi ya binadamu.

Amesema shirika hilo hufanya ukaguzi wa bidhaa viwandani na katika masoko ili kujiridhisha hali halisi ya soko na inapobainika uwepo wa bidhaa hafifu huondolewa sokoni na atakayekutwa na bidhaa hizo hulazimika kulipia gharama za uteketezaji.

Nae Mkaguzi wa TBS kanda ya kati Domisiano Rutahala amesema kawaida bidhaa za vyakula zikimaliza mda wake hugeuka sumu na miongoni mwa bidhaa zilizoteketezwa leo ni zile zenye viambata sumu ambavyo vikitumika husababisha madhara kwa mtumiaji hasa kwa wananwake huweza husababisha kuharibu mfumo wa uzazi.

Post a Comment

Previous Post Next Post