TPDC YAJIPANGA KUZALISHA GESI KWA WINGI PINDI MRADI WA MWALIMU NYERERE UTAKAPOMALIZIKA

 Naibu Waziri wa Nishati Mhe.Stephen Byabato akizungumza na waandishi wa habari leo baada ya kufanya ziara katika kituo cha Kinyerezi Gas Plant Jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Dkt.James Mataragio ziara ya Naibu Waziri wa Nishati Mhe.Stephen Byabato katika kituo hicho Jijini Dar es Salaam.Naibu Waziri wa Nishati Mhe.Stephen Byabato akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Dkt.James Mataragio katika ziara yake leo kwenye kituo cha Kinyerezi Gas Plant Jijini Dar es Salaam.

*************************************************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Kituo cha kuzalisha kuzalisha Umeme wa gesi ya Kinyerezi II (Kinyerezi Gas Plant) kimeweza kuzalisha gesi zaidi baada ya kufanikiwa kuzalisha futi za ujazo milioni 211 kiasi ambacho akijawahi kuzalishwa.

Ameyasema hayo leo Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Dkt.James Mataragio katika ziara ya Naibu Waziri wa Nishati Mhe.Stephen Byabato katika kituo hicho Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika Ziara hiyo Dkt.Mataragio amesema wanategemea kwamba Mwalimu Julius Nyerere itakapoanza kiasi cha gesi ambacho kitakuwa kimepunguzwa basi kitaenda kuzalisha bidhaa nyingine ambayo vilevile inaweza kuchangia ajira mbalimbali kwenye viwanda.

“Umeme unaozalishwa Tanzania asilimia 60 ya huo umeme unatokana na gesi ambayo inatoka gas plant hivyo Mwalimu nyerere itakapoanza kiasi cha gesi kitapungua kwahiyo tumejipanga kuna viwanda vimekuwa vikiomba gesi kwaajili ya kuendelesha mitambo yao kwa mfano viwanda vya mbolea pamoja na viwanda vya kemikali”. Amesema Dkt.Mataragio.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Nishati Mhe.Stephen Byabato ametoa pongezi kwa kituo hicho kwa kufanya kazi kwa weledi na kuzingatia kanuni za usalama kwenye neoe hilo hatarishi.

“Tunayo miundombinu ya thamani kubwa hapa tunajua shughuli zinazofanyika hapa ni hatarishi zinahitaji ufuatiliaji na uzingatiaji wa maelekezo mbalimbali na kwasababu mpaka leo hatujapata tatizo lolote tuna amini mmekuwa wazingatiaji wazuri wa maelekezo ambayo yako hapa mlifanya kazi kwa kujituma na uzalendo”. Amesema Mhe.Byabato.

Post a Comment

Previous Post Next Post