Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Jaji Mstaafu Thomas Mihayo (Kushoto) na Mshauri wa Utamaduni wa Ubalozi wa China na Mkurugenzi wa Utamaduni wa Kituo cha Utamaduni cha Watu wa China nchini Tanzania, Wang Sipera wakiweka saini wakati wa hafla hiyo iliyofanyika katika ofisi za TTB jijini Dar es salaa.
………………………………………………………………………….
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Jaji Mstaafu Thomas Mihayo pamoja na Mshauri wa Utamaduni wa Ubalozi wa China na Mkurugenzi wa Utamaduni wa Kituo cha Utamaduni cha Watu wa China nchini Tanzania, Wang Sipera tarehe 11 Januari, 2021 wameweka saini kadi maalum (Post Cards) kama ishara ya kupokelewa Tanzania na baadaye zitarudishwa nchini china ambapo zitakabidhiwa kwenye kampuni 17 zilizopo kwenye program maalum ya kutangaza utalii wa Tanzania katika soko hilo la utalii la China. Tukio hili lilifanyika katika ofisi za TTB jijini Dar es Salaam.
Katika kuendeleza jitihada za kutangaza utalii wa Tanzania nchini China, tarehe 21 Disemba 2020 Ubalozi wa Tanzania nchini China kwa kushirikiana na Makampuni 17 ya kusafirisha watalii wa ngazi za juu (High –end Tourists) ulizindua program maalum ya kutangaza utalii wa Tanzania kwa njia ya “Post Cards” kwa lengo la kuongeza idadi ya watalii kutoka katika soko la utalii la China kuja kuviembelea vivutio vya utalii vya Tanzania.
Kadi hizi zililetwa Tanzania kupitia mashirika ya ndege ya Ethiopia na Qatar . Tarehe 1 January 2021 Kadi hizi zilikabidhiwa kwa kampuni ya Fashion Tourism ya Tanzania waandaaji wa program hii ambayo iliandaa timu ya watu kuzipandisha mpaka kwenye kilele cha Mlima Kilimanjaro kama ishara ya upendo na kujali watu katika kipindi cha mwaka 2020 ambapo hawajaweza kusafiri nje ya China kwa sababu ya ugonjwa wa COVID 19 na mwaka mpya 2021 utakuwa ni wa Baraka na wataweza kufikia kilele cha matumaini yao.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Jaji Mihayo alisema, “Naupongeza Ubalozi wa Tanzania nchini China kwa juhundi wanazozifanya ya kuvumbua mbinu mpya ya kutangaza utalii wa Tanzania na huu ni mfano wa kuigwa wa kutumia mahusiano na mawazo mazuri yanayoletwa na wadau kwa manufaa ya nchi ya Tanzania. Naendelea kutoa rai kwa balozi za Tanzania nchi za nje, jumuia,taasisi na watu binafsi kuibua mbinu zingine zitakazoweza kusaidia kutanzangaza utalii wa Tanzania ili kufikia lengo la kufikisha idadi ya watalii 5,000,000 ifikapo 2025”.
Kwa upande wa Mshauri wa Utamaduni wa Ubalozi wa China na Mkurugenzi wa Utamaduni wa Kituo cha Utamaduni cha Watu wa China nchini Tanzania, Wang Sipera ameonyesha kuridhishwa na namna TTB inavyotoa ushirikiano kwa makampuni ya Kichina yanayotoa huduma za watalii nchini Tanzania, “Natamani kuona programu hii inakwenda vizuri, hii ni ishara nzuri kwa makampuni ya kichina ya yaliyopo Tanzania kupata watalii wengi kutoka china na kupewa huduma nzuri kipindi chote watakapotembelea vivutio vya utalii vya Tanzania. Pia naipongeza kampuni ya Fashion Tourism kwa simamia na kuhakikisha program hii inafanikiwa.
Meneja wa kampuni Fashion Tourism Bi. Doris Xuziqi tumeona tushirikiane pamoja na ubalozi wa Tanzania na makapuni ya watoahuduma ya utalii ya china kutumia mbinu hii ili watalii wa soko la hili waweze kupata hisia ya uzuri wa vivutio vya utalii vya asili vya Tanzania, na China itakapofungua mipaka yake watalii wa china waje kwa wingi kutembea Tanzania. Pia tunanawashukuru TTB, Serena Hotel, TAZARA namashirika ya ndege ya Ethiopia na Qatar kutushika mkono na kuweza kufanikisha tukio hili la leo