WAZIRI UMMY: TRA MSICHOKE KUTOA ELIMU YA MLIPA KODI

 

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Ummy Mwalimu katikati akizungumza leo wakati wa kikao cha Jukwaa la Wadau wa TRA mkoa wa Tanga kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella kushoto ni Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga Specioza Owure
MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella akizungumza wakati wa kikao hicho
KATIBU Tawala wa Mkoa wa Tanga Judica Omari akizungumza wakati wa kikao hicho

Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga Specioza Owure akizungumza wakati wa kikao hicho
MKUU wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa akizungumza wakati wa kikao hicho kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella kulia ni Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga  Abdurhamani Shiloo
KATIBU wa JWT Mkoa wa Tanga Ismail Masoud akizungumza jambo kwenye kikao hicho
AFISA Madini Mkazi wa Mkoa wa Tanga Zabibu Napacho akieleza jambo kwenye kikao hicho
Meneja wa Benki ya NMB  Tawi la Madaraka Jijini Tanga Elizaberth Chawinga akieleza jambo kwenye kikao hicho
Wadau wa kikao hicho wakifuatlia matukio mbalimbali
Wadau wa kikao hicho wakifuatlia matukio mbalimbali
Wadau wa kikao hicho wakifuatlia matukio mbalimbali

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Ummy Mwalimu ameitaka mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Tanga wasichoke kutoa elimu ya mlipa kodi kutokana na kwamba kodi ndio msingi na uhai wa maendeleo ya Taifa.

 

Ummy Mwalimu ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Tanga(CCM) aliyasema hayo leo wakati wa kikao cha Jukwaa la Wadau wa TRA Mkoa wa Tanga kilichofunguliwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella ambapo alisema suala la elimu kwa walipa kodi ni muhimu ili waweze kutambua umuhimu wake.

 

Alisema  suala la utoaji wa elimu ni muhimu sana na iendelee kutolewa kwa kila mtu yupo tayari kulipa kodi na tupo kutokana na maendeleo lakini kikubwa waendeele kutoa elimu ambayo itakuwa ni chachu kubwa ya kuweza kufikia malengo yao waliojiwekea ya ukusanyaji wa kodi.

 

“Ndugu zangu TRA mnafanya kazi kubwa na nzuri lakini msichoke endelee kutoa elimu na wanatambue umuhimu wa kulipa kodi kwa sababu msipotoa elimu kuna watu wanaingia kwenye gharama kubwa zaidi kutokana na ujanja ujanga na kwa sababu hawana elimu ndio wanakwepa kulipa kodi”Alisema

 

“Lakini pia kuna baadhi ya watumishi sio waaminifu kesho anakwenda anachukua elfu ishirini na siku inayofuatia elfu 50 jamani tubadilike tuachane na masuala hayo lazima tusisitze umuhimu wa kulipa kodi kwa wafanyabiashara “Alisema

 

Akizungumzia masuala ya makadirio, Waziri Ummy aliitaka mamlaka hiyo kuhakikisha wanatenda haki kwa kuangalia uhalisia wa biashara au huduma inayotolewa kwa sababu unaweza kumpa mtu makadirio ya bei ya juu badala ya kumsaidia ukidhani kwamba ndio utapata kodi kumbe hupati.

 

“Mkiwapa kodi ambayo ni halali watajua ni wajibu wao na wataweza lakini niwaambie kwamba Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt John Magufuli inawapenda walipa kodi na wafanyabiashara na nihimize kuhakikisha mnalipa kodi”Alisema

 

Awali akizungumza wakati akifungua kikao hicho Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella alisema ulipaji wa kodi ndio ute wa mgongo wa Taifa lolote hivyo hawana budi kujipanga vizuri kuhakikisha watumishi wa TRA na wafanyabiashara hawajengeani mazingira ya chuki

 

Alisema mazingira hayo yanatokana na wao kudhani watu wa TRA wanakuja na makadirio yasikuwa na utaratibu hivyo aliwataka kuhakikisha wanafanya biashara kwa uwazi na watoe ushirikianokwa  TRA na TRA wahakikishe wanaendesha shughuli zao kwa mujibu wa sheria na maadili ya utumishi wa umma.

 

Awali akizungumza katika kikao hicho Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga, Specioza Owure alisema kwamba hivi sasa watawakamata watu wasiodai risiti huku akieleza kwamba kampeni hiyo wanataka kuanzisha wakati wowote ule.

 

Akizungumzia lengo lao la ukusanyaji wa mapato kwa mwaka 2020/2021ambapo alisema kwa upande wa Idara za kodi za ndani inalengo la kukusanya Bilioni 66 na mpaka sasa wana asilimia 120 ya hilo lengo huku kodi za Forodha ikiwa ni bilioni 66 na asilimia 83 lakini kimkoa lengo kuu kukusanya Bilioni 138.9 hivyo wan kazi kubwa ya kufanya

Post a Comment

Previous Post Next Post