MARYPRISCA ATOA SIKU 14 KWA MENEJA WA RUWASA MKOA WA MBEYA KUKAMILISHA MIRADI YA MAJI VIJIJI SITA

 

*****************************************************

NAIBU Waziri wa Maji, Maryprisca Mahundi, ametoa siku 14 kwa Meneja wa Mamlaka ya Maji Vijijini (RUWASA) Mkoa wa Mbeya, Mhandisi Hans Patrick kukamilisha miradi ya maji katika vijiji sita vya Kata ya Iwindi katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya ili kuwaondolea wananchi wa vijiji hivyo kero ya upatikanaji wa maji.

Aidha Naibu Waziri ametoa mwezi mmoja kwa meneja huyo kukamilisha mradi wa maji wa vijiji viwili vya Kata ya Igale ambavyo havijawahi kupata maji ya bomba kutokana na Jiografia yake ya milima milima.

Ametoa agizo hilo baada ya wananchi wa Kata ya Iwindi kulalamikia tatizo la ukosefu wa maji ya bomba kutokana na miradi mitatu ya maji ambayo iligawanywa katika vijiji viwili viwili kutokamilika na hivyo kuwafanya waendelee kuteseka

Post a Comment

Previous Post Next Post