KATIBU MKUU MHANDISI ANTHONY SANGA AKUTANA NA BALOZI WA AUSTRIA NCHINI

 

Mazungumzo yakiendelea baina ya Katibu Mkuu, Wizara ya Maji Mhandisi Anthony Sanga na ugeni uliomtembea

Katibu Mkuu, Wizara ya Maji Mhandisi Anthony Sanga akifurahia jambo pamoja na Balozi wa Austria nchini Tanzania Dkt. Christian Fellner aliyefika ofisini kwake katika mji wa Serikali Dodoma. 

Katibu Mkuu, Wizara ya Maji Mhandisi Anthony Sanga akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Austria nchini Tanzania Dkt. Christian Fellner, na wafanyabiashara kutoka Austria alioambatana nao

Baadhi ya wafanyabiashara walioongozana na Balozi wa Austria nchini Tanzania Dkt. Christian Fellner wakiwa ofisini kwa Katibu Mkuu, Wizara ya Maji Mhandisi Anthony Sanga (hayupo pichani).

**********************************************

Katibu Mkuu, Wizara ya Maji Mhandisi Anthony Sanga amekutana na Balozi wa Austria nchini mwenye makazi yake nchini Kenya, Dkt. Christian Fellner ofisini kwake katika mji wa Serikali Dodoma.

Mhandisi Sanga amefanya mazungumzo na Balozi Christian aliyeambatana na baadhi ya wafanyabiashara wenye makampuni makubwa kutoka Austria, kwa lengo la kuangalia namna ya kushirikiana katika sekta ya maji.

“Kimsingi, tunaangalia sehemu ambazo tunaweza kushirikiana nao katika uwekezaji wa miundombinu ya maji, kupitia ugeni huo tunatafuta pesa za kujenga miradi ya maji,” Mhandisi Sanga, amesema.

Naye balozi Dkt. Christan Fellner amesema kwamba anamshukuru sana Balozi wa Tanzania nchini Kenya Balozi John Simbachawene kwa kuandaa na kuwezesha ujumbe wa wafanyabiashara hao kufika Tanzania na kufanikisha mazungumzo hayo.

Naye, Balozi Simbachawene amesema makampuni hayo 13 ya kimataifa kutoka Austria yamevutiwa katika masuala ya uwekezaji hapa nchini hususan maendeleo ya kuboresha miundombinu mbalimbali.

Post a Comment

Previous Post Next Post