Na Abdullatif Yunus Michuzi TV
NAIBU Waziri wa Nishati na Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini Adv. Stephen Lujwahuka Byabato, yupo Jimboni Bukoba Mjini kwa mara ya kwanza tangu kuapishwa kushika wadhifa wa nafasi ya Naibu Waziri wa Nishati
Mhe. Byabato ambaye kupo Mkoani Kagera kwa shughuli za Kiserikali, katikati ya Wiki hii amepata nafasi ya kuzungumza na Wananchi wa Jimbo lake katika Mkutano wa Hadhara uliofanyika maeneo ya Soko kuu la Bukoba, Mkutano ambao Mhe. Byabato ameainisha Mambo sita aliyoamua kuyafanya kwa Wanajimbo lake licha ya kuwa muda ni mchache tangu Wanajimbo hao kumpa ridhaa ya kuwa Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini.
Mambo hayo Sita aliyoyafanya na anayokusudia kuyafanya Kwanza, Mhe. Byabato katika kuunga Juhudi za Elimu na kuhakikisha Februari Wanafunzi waliofaulu kuanza Kidato cha Kwanza wanaingia Madarasani, Mhe. Byabato atakabidhi
Mifuko 140 ya saruji kwa ajili ya Ujenzi wa Vyumba vya Madarasa kwa Shule za Sekondari, kwa Kata zote 14 zinazounda Jimbo la Bukoba Mjini, na kila kata itapata Mifuko 10.
Aidha Jambo la pili Mhe. Byabato meongeza kuwa ni kuhusu Elimu, wapo Watoto wanaotoka familia zisizojiweza na wanatakiwa Januari kuanza Masomo yao, hivyo ametoa Sare za Shule kwa Wanafunzi 20 kila Kata, na Kufanya idadi ya sare zipatazo 280 zitakazotolewa kwa jumla ya kata zote 14, Sare ambazo zitagawiwa kwa Utaratibu maaulum unaoendelea kuratibiwa chini ya Ofisi ya Mbunge.
Jambo la Tatu ambalo Mhe. Byabato amefanya, ni kutoa Shukrani zake kwa Mema ambayo Mwenyezi Mungu amemtendea kipindi hiki, shukrani hizo akiziwasilisha kwa namna ya kula Sikukuu ya Krismasi na Watoto yatima wa Vituo Viwili vya kulelea Watoto hao, ambavyo ni Kituo Cha kulea Yatima cha NUSURU YATIMA cha Kata Kashai, na kile cha TUMAINI JIPYA cha Kata Nyanga, ambapo Mhe. Byabato ametoa Mkono wa Sikukuu kwa Vituo hivi kwa kuwapeleka zawadi ya chakula na Vinywaji.
Aidha jambo la Nne ambalo litafanywa na Mhe. Mbunge Byabato Jimboni kwake, Ni pamoja na ukarabati wa Soko Kuu la Bukoba sehemu moja ya Wauza Ndizi, ambapo eneo hilo huwa kero nyakati za Mvua, kwa kujaa tope Jambo ambalo husababisha adha kubwa kwa wachuuzi na wanunuzi wa Ndizi. Mhe. Byabato ameomba Wachuuzi hao wamkubalie kifusi na kujenga Mitaro ili kuboresha eneo hilo, shughuli ambayo itaanza Mara tu baada ya kukubaliwa kwani shughuli hiyo inaweza kuathiri kwa muda hali ya Biashara wakati wa ukarabati.
Jambo la Tano ambalo Mhe. Byabato amelifanya, ni Kumteua na kumtangaza Hadharani msaidizi wake ambaye Ni Katibu wa Mbunge atayekuwa anashughulika na Shughuli zote za Ofisi ya Mbunge, lakini pia akiwa kiunganishi Kati ya Mbunge na Wananchi kipindi ambacho Naibu Waziri huyo wa Nishati atakuwa Nje ya Jimbo akitekeleza Majukumu mengine ya Kitaifa. Katibu huyo Mhandisi Pasaka K. Bakari tayari ameanza majukumu yake Rasmi Mara baada ya kutangazwa Jambo ambalo kwa muda Sasa lilikuwa kitendawili.
Jambo la Sita ambalo Mhe. Byabato amefanya ni Uwezeshaji wa Gari la Jimbo, ambapo Mhe. Byabato kwa pesa yake amenunua Usafiri aina ya Gari, Basi Dogo la Abiria lenye Namba za Usajili T 946 DVA na kulizinduwa Mkutanoni, Gari hilo litahusika moja kwa Moja katika Jimbo lake kwa Shughuli za Kijamii kama Misiba, Ugonjwa na Shughuli za Dharula, na kuomba Wananchi kulitunza Gari hilo kwa Matumizi ya Jimbo, huku Gari hilo likionekana kunakishiwa kwa maandishi mbalimbali na picha tofauti huku maaandishi makubwa yakisomeka ubavuni "Jimbo letu, Usafiri Wetu