WIZARA YA MAJI KUMALIZA MKIRADI YOTE YA MAJI SONGEA

 

Katibu Mkuu wa wizara ya Maji Mhandisi Anton Sanga kulia na Mbunge wa Jimbo la Peramiho Jenista Mhagama katikati wakimtwisha ndoo ya maji  jana mkazi wa kijiji cha Litisha jimbo la Peramiho wilayani Songea  Anna Mwingira  mara baada ya katibu mkuu huyo kutembelea mradi wa maji katika kijiji hicho ambapo ameridhishwa na utekelezaji wake.

Picha na Muhidin Amri

………………………………………………………………………………….

Na Mwandishi Wetu,Songea

SERIKALI imesema,ina fedha za kutosha kwa ajili ya kukamilisha miradi ya maji katika maeneo mbalimbali hapa nchini ikiwa ni mkakati wake  wa kumaliza kero ya maji kwa wananchi.

Kauli hiyo ya serikali imetolewa jana na katibu Mkuu wa wizaya ya maji Mhandisi Anton Sanga mara baada ya kukagua ujenzi wa mradi wa maji katika kijiji cha Litisha wilayani Songea unaotekelezwa na wakala wa maji vijijini Ruwasa na kujengwa na Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira manispaa ya Songea(Souwasa).

Aidha Sanga,amewahakikishia wananchi wa jimbo la Peramiho wilaya ya Songea mkoani Ruvuma kuwa,tatizo ya maji linalowakabili  wananchi wa jimbo hilo litakwisha katika kipindi cha miezi miwili kuanzia sasa.

Katika kuthibitisha ya serikali,Sanga amehaidi kutoa shilingi milioni 200 wiki ijayo kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa mradi mkubwa wa maji katika kijiji hicho ambao ujenzi wake umefikia asilimia 85.

Amesema, mradi huo utakamilika haraka iwezekavyo ili wananchi wa Litisha waweze kupata maji kwani wamechoka kusubiri huduma hiyo kwa muda mrefu na kwamba hata  Rais Magufuri amedhamiria kumaliza kero ya maji katika maeneo yote hapa nchini.

Sambamba na hilo Sanga amewataka watendaji wa wizara ya maji kuhakikisha wanatekeleza miradi ya maji kwa weledi na kujiepusha na vitendo vinavyoweza kukwamisha juhudi zinazofanywa na serikali zinazolenga kuboresha maisha ya Watanzania.

Pia ameagiza wataalam hao kuanza  mchakato wa kuwaunganisha maji wananchi wa kijiji hicho  majumbani kwani ndani ya siku sitini mradi utakamilika,hivyo sio vema wasubiri hadi maji yatakapoanza.

Kwa upande wake,Mbunge wa jimbo la Peramiho Jenista Mhagama ameishukuru serikali kwa usimamizi na utekelezaji mzuri wa miradi ya maji katika vijiji mbalimbali katika jimbo hilo,hata hivyo ameiomba wizara kukamilisha baadhi ya miradi ambayo bado haijakamilika.

Alisema, katika jimbo hilo kuna miradi 19 kati ya hiyo ni miradi 9 tu iliyokamilika na wananchi wanasubiri sana kuona maji yanapatikana katika maeneo yao.

Alisema, wakati wa kampeni ya uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba changamoto kubwa iliyojitokeza kwa wananchi wa jimbo hilo ni  ukosefu wa huduma ya maji safi na salama,kwa hiyo wizara ya maji ione umuhimu wa kumaliza kilio hicho cha wananchi ambao wana shauku kubwa ya kupata maji.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya Songea Menas Komba amemshukuru katibu mkuu kwa uamuzi wake wa kufika jimbo la Peramiho kuangalia utekelezaji wa miradi  ya maji na kuhaidi kuwa,miradi hiyo itatunzwa ili iweze kudumu kwa kizazi cha sasa na kijacho.

Alisema, jimbo la Peramiho ni kati ya maeneo yenye changamoto kubwa ya maji na kuiomba wizara hiyo kuhakikisha inakamilisha miradi yote iliyoanza kutekelezwa ili wananchi wasipoteza tena muda wao kutafuta maji badala yake watumie muda kufanya shughuli za kujiletea maendeleo.

Post a Comment

Previous Post Next Post