Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Nadhifa Kemikimba akifungua Kongamano la 8 la Maji jijini Dodoma.
Baadhi ya washiriki wa Kongamano la 8 la Maji wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Nadhifa Kemikimba (hayupo pichani) wakati akihutubia kwenye Kongamano hilo jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Nadhifa Kemikimba (kushoto) akimsikiliza Mwanafunzi wa Chuo cha Maji, Daudi Sangi akitoa maelezo kuhusu ufanyaji kazi wa pampu ya kusukuma maji alipotembelea mabanda ya Maonesho ya Wazabuni katika Kongamano la Maji la 8 jiiini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Nadhifa Kemikimba akiwa na wajumbe wa meza kuu katika Kongamano la Maji la 8 jiiini Dodoma.
Mwenyekiti wa Bodi ya ATAWAS, Mhandisi Geofrey Hilly akitoa taarifa ya utendaji wa taasisi hiyo katika Kongamano la Maji la 8 jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Nadhifa Kemikimba (kushoto) akisalimiana na miongoni mwa Wadau wa Maendeleo walioshiriki Kongamano la Maji la 8 jijini Dodoma.
****************************************
Naibu Katibu Mkuu, Mhandisi Nadhifa Kemikimba ameitaka Jumuiya ya Wasambazaji Maji Tanzania (ATAWAS) kutoa kipaumbele kwenye eneo la majitaka baada ya kufanikiwa kwa kiasi kikubwa kwenye eneo la usambazaji wa majisafi.
Mhandisi Kemikimba ametoa maelekezo hayo katika uzinduzi wa Kongamano la 8 la Maji katika ukumbi wa mikutano wa St. Gasper, jijini Dodoma.
“Kuna mafanikio makubwa kwa upande wa usambazaji maji, lakini kwa upande wa majitaka bado. ATAWAS mnatakiwa kuwekeza kiasi kikubwa kwenye eneo hili, ambapo lengo letu ni kufikia asilimia 30 ifikapo mwaka 2025 kwa sababu majisafi ni mengi na itachangia kuwepo kwa majitaka mengi “, amezungumza Naibu Katibu Mkuu.
“Serikali ipo tayari kutoa ushirikiano ili kufanikisha azma hiyo, lakini pia ni lazima katika majadiliano yenu muweke msisitizo kwenye utafiti na ubunifu kwa kuwatumia Taasisi za Elimu ya Juu ili kuweza kupata suluhisho la kudumu litakalomaliza changamoto zote”, amesisitiza Mhandisi Kemikimba.
Kadhalika, Naibu Katibu Mkuu ametoa wito kwa wadau wote wa Sekta ya Maji nchini kushirikiana na ATAWAS ili kufanikisha utekelezaji wa miradi ya maji kwa sababu peke yao hawatafanikiwa.
Aidha, Mwenyekiti wa Bodi ya ATAWAS na Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Tanga (Tanga UWASA), Mhandisi Geofrey Hilly amesema ATAWAS imezindua rasmi mpango wa kuwajengea uwezo wanachama wake kwenye eneo la menejimenti ya rasilimali fedha, ukizingatia kuwa miongoni mwa changamoto kubwa ambazo zinazozikabili Mamlaka za Maji na sekta kwa ujumla, ni usimamizi wa fedha za utekelezaji wa miradi mijini na vijijini.
Pia, ameongeza kuwa ATAWAS pamoja na Taasisi za Elimu ya Juu zimeshasaini mkataba wa ushirikiano kwenye eneo la utafiti kwa lengo la kupata suluhisho la kudumu changamoto za kisekta.
Lengo la Kongamano hilo ni kujadiliana, kutathimini na kuzipatia ufumbuzi changamoto za kisekta na kubaini fursa zilizopo ili kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kufikia dira ya Taifa ya mwaka 2025, pamoja na lengo la sita (6) la Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa kwa mwaka