WATUMISHI WA GST WAPEWA SEMINA ELEKEZI JUU YA MAADILI YA UTUMISHI WA UMMA

  Samwel Mtuwa - GST


Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Profesa Simon Msanjila leo septemba 5 , 2020 amefungua semina elekezi kwa watumishi wa Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST).

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina Katibu Mkuu Profesa Msanjila aliwasii watumishi wa GST juu ya kuzingatia Sheria , kanuni , maadili na maadili na taratibu za utumishi wa umma ikiwa pamoja na kuzingatia muda wa  kazi, uwajibikaji mahali pa kazi, umuhimu wa mawasiliano baina ya kiongozi na kiongozi,utunzaji bora wa nyaraka za Serikali , umuhimu wa kuomba ruhusa mahali pa kazi na mtumishi kuzingatia mavazi sahihi ya utumishi.

Awali Mtendaji Mkuu wa GST Dkt.Mussa Budeba akimkaribisha katibu Mkuu kwa ajili ya ufunguzi wa semina aliwaomba watumishi kuwa wasikivu na kufuatilia mada zote zitakazo wasilishwa na wawezeshaji kwa lengo la kuleta mabadiliko katika utendajikazi ndani ya taasisi.

Akizungumzia juu ya umuhimu wa taasisi za Utafiti , Profesa Msanjila alisema GST inatakiwa kujiendesha kwa Utafiti kwa kushirikiana na taasisi nyingine za utafiti wa jiolojia zilizo ndani ya nchi na zile zilizo nje ya nchi kwa kuzingatia usawa wa mafanikio kwa pande zote mbili yaani (win-win situation).

Semina hii elekezi juu ya maadili ya Utumishi wa Umma imefanyika kwa lengo la kuwajengea uwezo watumishi wa GST pamoja na kuboresha utendajikazi ndani ya taasisi.

Pamoja na Katibu Mkuu wengine waliotoa mada za uwezeshaji ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu kutoka Wizara ya Madini Ndugu Issa Nchasi pamoja na Jussein Mwakipesile kutoka Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Profesa Simon Msanjila akizungumza wakati wa kufungua semina watumishi wa GST juu ya kuzingatia Sheria , kanuni , maadili na maadili na taratibu za utumishi wa umma ikiwa pamoja na kuzingatia muda wa  kazi, uwajibikaji mahali pa kazi, umuhimu wa mawasiliano baina ya kiongozi na kiongozi,utunzaji bora wa nyaraka za Serikali , umuhimu wa kuomba ruhusa mahali pa kazi na mtumishi kuzingatia mavazi sahihi ya utumishi.
Mtendaji Mkuu wa GST Dkt Mussa Budeba akizungumza na watumishi wa GST hawapo pichani pindi alipokuwa akimkaribisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Profesa Simon Msanjila kufungua semina
Baadhi ya watumishi wakifuatilia semina



Post a Comment

Previous Post Next Post